Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) akikiri kuupokea Mwenge wa
Uhuru wa mwaka 2019 baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia.
Jenerali. Mstaafu Nicodemus Mwangela (kushoto).
Mwenge wa Uhuru wa Mwaka 2019 utakaokimbizwa katika wilaya
tatu na Halmashauri Nne za Mkoa wa Rukwa unategemewa kuweka Mawe ya Msingi, kukagua
na kuzindua miradi 35 ya maendeleo pamoja na vikundi 11 vya wanawake, vijana na
watu wenye ulemavu ambapo miradi hiyo ina thamani ya Shilingi Bilioni 45,404,104,489.59.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
baada ya kukabidhiwa mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia. Jenerali.
Mstaafu Nicodemus Mwangela mara tu baada ya kuvuka daraja la mto Momba mbao
ndio mpaka wa Mkoa wa Rukwa na Songwe katika Kijiji cha Kilyamatundu, Wilayani
Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Mwenge wa uhuru ukiwa katika
Mkoa wa Rukwa utakimbizwa umbali wa jumla ya Kilomita 832.5 kuanzia tarehe 7
hadi 11, April, 2019 nahatimae kuwakabisdi majirani Mkoa wa Katavi, ambao
utakuwa mkoa wa tatu tangu kuwashwa kwake katika mkoa wa Songwe mapema mwezi
huu.
Wakati akifafanua
michanganuo ya uchangiaji wa miradi hiyo Mh. Wangangabo alisema “Wananchi Shilingi
244,524,500.00 sawa na asilimia 0.5 ya gharama zote.Halmashauri Shilingi 619,611,106.00
sawa na asilimia 1.4, Serikali Kuu Shilingi 16,426,480,402.00 sawa na asilimia 36.2,
Wadau wa maendeleo Shilingi 759,489,800 sawa na asilimia 1.7 Aidha, kuna mradi wa
uchimbaji makaa ya mawe ambao unathamani ya Shilingi 27,353,998,681.59 mradi
huu utakaguliwa, ambao una wastani wa asilimia 60.2 ya gharama zote.”
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
mwaka 2019 aliupongeza uongozi wa mkoa wa Rukwa kwa mapokezi mazuri aliyoyapata
na kuwaahidi kutowaangusha wananchi katika ukaguzi wake wa miradi ambayo Mwenge
wa Uhuru utaipitia.
Kauli
mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 ni “Maji ni haki ya kila Mtu, tutunze vyanzo vyake na
tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
No comments:
Post a Comment