HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 08, 2019

Ngorongoro Race kufanyika Aprili 20

Kaimu Meneja Mahusiano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joyce Mgaya, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wao kuelekea mbio za Ngorongoro Race zitakazofanyika Karatu Aprili 20. Kushoto ni Mratibu wa Ngorongoro Race, Meta Petro. (Picha na Tullo Chambo). 

ARUSHA, Tanzania
 
Watanzania wametakiwa kjitokeza kwa wingi kuweza kutembelea Mbuga za wanyama lakini pia kushirki katika mbio za Ngorongoro race zitakazofanyika Aprili 20 kwa lengo la kuhakikisha ya kuwa jamii inaendelea kufahamu kwa kina kuhusu maana halisi ya utalii wa Tanzania.

Wito huo umetolewa leo katika ofisi za Ngorongoro jijini Arusha na mwendeshaji wa mbio za Ngorongoro Race Bw, Metha Petro wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio hizi.

Aidha Bw, Metha Petro aliwashukuru Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kudhamini mbio hizi toka zilipo anza rasmi mwaka 2008 mpaka sasa ambapo wamekuwa ni mchango mkubwa katika uwepo wa mbio hizi, lakini pia amefafanua kwa kina kuhusu hizi mbio ambapo alisema zipo mbio za kilometa ishirini na moja zitakazo anzia katika geti la Ngorongoro, mbio za kilometa tano ambazo zitaanza katika maeneo ya Baishai na mbio za kilometa mbili na nusu kwa ajili ya watoto zitakazo anzia ilipo ofisi ndogo ya Ngorongoro.

Sanjari na hayo aliongeza ya kuwa wamefika katika hatua ya mwisho ambapo wana matarajio ya washiriki zaidi ya elfu moja watakao shiriki mbio hizi lakini pia usajili utaanza rasmi siku ya jumatano ya tarehe kumi ya mwezi huu na sutafanyika katika vituo viwili tofauti ambavyo ni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid , ofisi ya Gidabuday iliyoko jijni Arusha pamoja na ofisi ya Ngorongoro race iliyoko Karatu mjini.

Kwa upand wake Kaimu Meneja wa mawasiliano Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro B,i Joyce Mgaya alisema ya kuwa kwa mara nyingine tena mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imedhamini mbio hizi kwa lengo la kuhakikisha ya kuwa wanahamasisha utalii wa ndani na kujenga mahusiano mazuri na wananchi na jamii kwa ujumla kwa lengo la kuhakikisha ya kuwa wanatembelea hifadhi hizo kwa gharama nafuu ambapo watu wazima ni sh. Elfu kumi na moja na mia nane na watoto ni shilingi elfu tano na mia saba kama kiingilio.

Vile vile Kaimu Meneja wa mawasiliano ya hifadhi ya Ngorongoro Bi, Joyce Mgaya amehitimisha kwa kusema watu mia moja watakao wahi kujiandikisha katika kuhudhuria mbio hizi watapata fursa ya kipekee ya kuweza kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tarehe 21 siku ya Pasaka.

No comments:

Post a Comment

Pages