NA JOHN MARWA
LICHA ya suluhu waliyoipata Simba SC katika mchezo
wao wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL jumamosi iliyopita
dhidi ya TP Mazembe Nyota wa Bongo Fleva ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo
Ommy Dimpoz bado anaamini watapenya nusu fainali.
Dimpozi amesema watu wasiichukulie poa Simba kwani
mpira una maajabu yake hivyo wanapaswa kutunza maneno yao na kusubiri dakika 90
za Lubumbashi.
Simba walitoka sare ya kwanza msimu huu katika
Uwanja wa Taifa wakitoka kushinda mechi tano mtawalia kabla ya kuzuiwa na
Mazembe kwa kushindwa kupachika bao mbele ya miamba hiyo ya Afrika.
Lilikuwa ni pambano la kwanza na mtanange wa pili
utapigwa siku ya jumamosi mjini Lubumbashi nchini Congo DR nyumbani kwa TP
Mazembe ambao watahitaji ushindi ili kusonga mbele.
Simba licha ya kuhitaji ushindi katika kabumbu hilo
la marejeano kama watapata sare ya mabao kwao utakuwa ni ushindi utakao
wapeleka nusu fainali japo sio kazi nyepesi dhidi ya mabingwa hao mara tano wa
michuano hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Omary Nyemo Ommy
Dimpoz alisema lolote linawezekana katika mchezo wa soka hivyo anaamini Simba
inaweza kupata matokeo na kusonga mbele kama watatimiza majukumu yao
kikamilifu.
“Kama wao walijipanga na kuweza kupata sare na sisi
tunaweza kujipanga na kupata ushindin Lubumbashi, tunaamini tunacheza na klabu
kubwa katika haya mashindano pia wao ni mabingwa mara tano hivyo wanauzoefu na
hii michuano.
“Mwanzo lengo la Klabu lilikuwa kufika hatua ya
makundi lakini tumevuka lengo tumefika hataua ya robo fainali bado tunaamini
tutajipanga mpira ni dakika 90 kuna watu hawakutegemea Simba kufika hapa lakini
wako wapi, Alhy kapigwa tano huko sio kwamba hajui ndo mpira. Alisema na
kuongeza kuwa,”alisema na kuongeza kuwa.
“Penati anakosa mtu yeyote wanakosa akina Messi na Ronaldo
kwanini watu wamlaumu Bocco inawezekana ikatugahrimu lakini ndio mpira.
“Yawezekana tungeshinda 4-0 hapa na kule tukapigwa 5-0
tusingeweza kusonga mbele lakini yawezekana tukawafunga bao moja kwao na
wakashindwa kuchomoa na Simba kusonga mbele.
“Katika hatua hii lazima mmoja atoke hivyo hata kama
tutatoka ndio mpira ila Imani yangu ni kubwa sana Simba tunaweza kusonga mbele.
Aliongeza kuwa mafanikio ya Simba yameweza kuliinua
soka la Tanzania yamerejesha hamasa kwa watanzania, na wameanza kujiamini kuwa
timu zao zinaweza kupata matokeo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa Taifa Stars kufuzu AFCON.
Pia alitoa rai yake kwa watanzania kuelekea
mashindano ya vijana ya afrika ambayo Tanzania ni wenyeji kupitia Serengeti
Boys
“Kuna umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kutoa hamasa
kwa vijana wetu lakini pia kama nchi tukijitokeza kwa wingi inaweza kutujengwea
Imani na kupewa nafasi nyingine kwa michuano mikubwa zaidi hivyo hii ni fursa itumike
vema vema.
“Michuano hii itatufanya tutembee vifua mbele kwenye
mataifa ya watu tukijivunia kuandaa michuano mikubwa ya AFCON kwa vijana Afrika,”alisema.
No comments:
Post a Comment