Mjumbe Kamati Tendaji RT-Habari na Mawasiliano, Tullo Chambo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa kuhusu maandalizi ya mbio za Sokoine Marathon. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Ufundi ya RT, Rehema Killo.
Mjumbe Kamati Tendaji RT-Habari na Mawasiliano, Tullo Chambo, akizungumzia mbio za Sokoine
Memorial Marathon 2019 zitakazorindima Aprili 6 jijini Arusha. Kushoto ni Katibu
Kamati ya Ufundi RT, Rehema Killo na kulia ni Katibu Kamisheni ya Wachezaji RT, John Jilala.
Dar es Salaam, Tanzania
NYOTA wa riadha nchini wametakiwa kujitokeza kuchuana kwenye
mbio za Sokoine Marathoni zitakazofanyika Machi 6 jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika mbio
hizo za kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine
itakayoadhimishwa Aprili 12.
Mjumbe wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Tullo Chambo
alisema mbio hizo zitashirikisha wanariadha nyota nchini na wengine kutoka nje
ya nchi ambao watakuwa na vibali kutoka kwenye Mashirikisho ya riadha ya nchi
wanazotoka.
"Mashindano yataanzia kwenye mnara wa Clock Tower
jijini Arusha na yatamalizikia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo
zitapokelewa na Waziri Mkuu Majaliwa, alisema Tullo.
Katibu wa Kamati ya Ufundi ya RT, Rehema Killo alisema
kutakuwa na mbio za kilomita 21 (Wazalendo nusu marathoni) ambazo washindi kwa
wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh 1 Milioni.
Alisema mshindi wa pili atazawadiwa Sh 800,000 na wa tatu Sh
600,000 huku zawadi zikitolewa kwa washindi 15 wa kwanza.
Alisema katika mbio hizo pia, wanariadha 500 wa kwanza kila
mmoja atapewa medali ya ushiriki. "Kwenye mbio za kilomita 5, kutakuwa na zawadi ya
medali na mbio za watoto za kilomita 2.5 mshindi atapewa Sh 100,000 kwa
msichana na mvulana na washindi 15 wa kwanza pia watapewa fedha Taslimu. Alisema mbio hizo zinafanyika kwa ushirikiano wa RT,
Serikali na Taasisi ya Sokoine.
Awali mbio hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza miaka minne iliyopita na msimu huu zitafanyika kwa mara ya pili ambapo zinalenga kumuenzi hayati Sokoine.
"Hatuna cha kumpa zaidi ya kuyaenzi yale matendo yake
aliyofanya Enzi za uhai wake," alisema Killo huku akitoa wito kwa
wanariadha kujitokeza kwa wingi kushiriki.
No comments:
Post a Comment