Angela
Karashana, ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza kuhusu mbio za Selous 2019,
zitakazofanyika mkoa wa Morogoro.
NA
MWANDISHI WETU
Msanii
wa Bongo Fleva nchini, Barnaba Eliasa 'Barnaba Boy', pamoja na Msanii
wa vichekesho Tabu Mtingita, kuongoza mbio za Selous Marathon zitakazo
fanyika Agosti 24 mkoani Morogoro.
Akizungumza kwa niaba
ya waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Angela
Karashana alisema kuwa mchezo wa riadha unamahusiano makubwa na burudani uwezi
kucheza au kukimbia bila kuburudika ndio sababu tunawaona wasanii wako kwa kuweza
kutuburudisha tunapomaliza kukimbia.
"Mtoto anapokuwa
tumboni mama lazima uulizwe mwanao anacheza tumboni, kwa kuwa kucheza kuna
hashiria uhai, Wapo watu wanatamani wapate nafasi ya kutembea tu na hawapati
wewe mwenye nafasi hii unaitajika kushiriki mbio za Selous 2019 kuna Wat u
watashangaa kwa nini Barnaba na Tabu wanashiriki ni kutokana na kuwa watu
wanakimbia umbali mrefu watu wa rika tofauti na wakimaliza kukimbia wanaitaji
kutuburudisha na kufurahia walichokifanya mbio zitafanyika Morogoro Watu
wajitokeze tukimbie kwa pamoja na michezo mbalimbali itakuwepo"anasema
Karashana.
Kwa upande wake mkali
huyo wa Bongo Fleva anasema yupo tayari kukimbia na watu wa Morogoro leo
tumezindua rasmi kadri tunavyoendelea watu wafate taratibu na kujiandikisha
kushiriki mbio hizi ili tuweze kukimbia na kuburudika kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment