Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akiwasili katika eneo la Kiwanda na Shamba la Miwa Mbigiri
linalohudumiwa na Gereza la Mbigiri wakati wa ziara ya kutembelea mradi
huo mkoani Morogoro. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Serikali imetoa onyo kwa wafanyabiashara au mtu yoyote mwenye nia
ya kuhujumu Miradi ya Serikali kwa maslahi binafsi kuacha mara moja na
endapo mtu atathibitika kuhusika na
suala hilo sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni leo alipotembelea Kiwanda na Shamba la Miwa katika Gereza la Mbigiri ambalo linakadiriwa kuzalisha tani za sukari Laki Mbili kwa Mwaka na kuondoa adha ya kuagiza sukari nje ya nchi.
Amesema Serikali ya
Awamu ya Tano imedhamiria kukuza viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha Sukari
Mbigiri na kuwezesha mamia ya wananchi kupata ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
“Kuna taarifa za baadhi
ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari kupenyeza maslahi yao binafsi katika
miradi hii mikubwa ya serikali ikiwemo shamba hili la miwa hapa Mbigiri, nawaasa
waache mara moja kwani watakapobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu
yao ikiwemo na kosa la uhujumu uchumi” alisema Masauni
Akitoa taarifa ya shamba
hilo Mkuu wa Gereza Mbigiri, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Shija Fungwe alisema
shughuli zinaendelea katika shamba hilo kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa
kutoka katika gereza hilo huku wafungwa 280 wakitumika katika shamba hilo.
“Kazi
ya kupanda eneo lililo tayari inaendelea huku kazi ya kulima hekta 500
inaendelea na kati ya hizo hekta 200 zimeshalimwa kwa awali na lengo letu
ikifika mwezi juni mwaka huu inatakiwa zilimwe hekta 700 tukitumia nguvu kazi
ya wafungwa” Alisema ACP Fungwe
Katika hatua nyingine
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameelekeza kubadilishwa kwa Mjumbe wa Bodi ya Kiwanda hicho, ACP Rocky
Mbena anaewakilisha Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment