Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawpo pichani) jana jijini Dodoma kuhusu namna ofisi yake imejipanga
kutumia jukwaa la mashindano ya AFCON U17 kutangaza fursa za utalii zilizopo
nchini katika kipindi cha mashindano hayo yatakayofanyika hivi karibuni nchini,
kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Bibi.Susan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) Bw.Wilfred Kidao. (Picha na Anitha Jonas – WHUSM).
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akitoa shukrani kwa
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa
kutoa fedha kiasi cha Bilioni Moja za
kuendesha mashindano ya AFCON U17 yatakayofanyika
hivi karibuni jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa
habari (hawapo pichani) jana jijini Dodoma, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda.
Katibu Mkuu Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidao (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jana
jijini Dodoma kuhusu aina ya wageni wanaotarajiwa kufika katika mashindano ya
AFCON U17 yatakayofanyika nchini hivi karibuni ambapo alieleza Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni Infantino anatarajia kuja katika
mashindano hayo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf
Mkenda.
No comments:
Post a Comment