NA MWANDISHI WETU
WANAFUNZI watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
wameibuka kidedea baada ya kufanikiwa kutengeneza njia ya kupeleka elimu kwa
njia ya mtandao kupitia Kampuni ya Vodacom Foundation Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya
kuwakabidhi zawadi wanafunzi hao, Meneja wa Ruzuku na Mawasiliano wa kampuni
hiyo, Sandra Oswald, alisema njia waliyobuni wanafunzi hao itawasaidia
wanafunzi wa vijijini kujisomea.
Aliwataja washindi hao kuwa ni John Alfred, Kevin Richard
wanaosoma mwaka wa tatu na Essa Mohamedali wa mwaka wa kwanza chuoni hapo.
Oswald alisema washindi hao wametokana na wiki ya ubunifu
iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) ambapo walipata
fursa ya kukaa na jopo la wabunifu wengine chini ya uongozi wa Vodacom Foundation
na kubadilishana ujuzi kisha kupatakikana kwa washindi hao.
“Tumekaa na wabunifu 27 kwenye makundi tisa ya watu watatu
watatu, tukawaambia nia yetu ni kupeleka elimu kwa watoto wote wa shule za
sekondari bila kwa njia rahisi, wanafunzi wapate vitabu kwa njia ya mtandao na mitaala
ya masomo yao wapate bure yaani mtu awe na bando tu.
“Tulikuwa na majaji wanne waliochambua kazi za wabunifu hao
hadi kuwapata washindi hawa leo… tulilenga kuwapata wabunifu wachanga ambao
hawana zaidi ya miaka mitano kwenye soko.
“Majaji walikuwa Jumanne Mtambalike, Muzafar Kaemdin,
Greyson Julius na Isaack Shayo. Waliangalia zaidi urahisi wa teknolojia
iliyobuniwa, ubora wa ubunifu, gharama nafuu na uharaka wa teknolojia
iliyobuniwa.
“…Washindi wamepata kompyuta mpakato na kubwa zaidi watapata
fursa ya kufanyakazi ya Vodacom Foundation,” alisema Oswald.
No comments:
Post a Comment