Mkurugenzi wa Amana Benki Dk.Muhsin Masoud, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya Halal Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za M-Pesa Vodacom, Tulisindo Rashid akizungumza huduma hiyo ya Halal Pesa itakavyofanya kazi.
Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa M-Pesa, Polycarp Ndekana, akizungumza katika uzinduzi wa halal pesa uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Na Suleiman Msuya
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za M-Pesa Vodacom, Tulisindo Rashid akizungumza huduma hiyo ya Halal Pesa itakavyofanya kazi.
Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa M-Pesa, Polycarp Ndekana, akizungumza katika uzinduzi wa halal pesa uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Na Suleiman Msuya
BENKI ya Amana kwa kushirikiana na Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom wamezindua huduma mpya ijulikanayo kama ''Halal Pesa''.
Huduma
hiyo mpya sasa itapatikana kwa wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa na
wale wa Amana Bank kwa kuzingatia misngi ya sheria ya kiislamu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Amana Bank, Dkt.
Muhsin Masoud, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakifikiria jinsi ya
kuwafikia wateja wengi zaidi ambao wanapenda kutumia miamala ya kifedha
kwa mujibu wa sheria ya kiislamu.
Dkt.
Masoud alisema Amana Bank imekuwa ikibuni njia mbalimbali za kuwafikia
wateja wake wazamani na wapya hivyo wameweza kuanzisha huduma hiyo ya
halal pesa ambapo wateja wa Vodacom wanaotumia M-pesa wataipata huduma
hiyo mpya inayozingatia misingi ya sheria ya kiislamu.
Alisema
katika huduma ya halal pesa mteja wa Amana Bank anaweza kufanya miamala
yake kwa kutumia Vodacom M-Pesa huku akiwa bado yupo kwenye sheria za
uislamu kuhusu miamala ya kifedha.
Dkt. Masoud alisema Amana Bank imetimiza miaka nane ikiendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria za kiislamu.
Alisema Benki hiyo ndio benki pekee hapa Tanzania ambayo mfumo wake wa kifedha umesimamia sheria za benki za kiislamu.
Hata
hivyo alisema licha ya Benki hiyo kufuata sheria za kiislamu katika
uendeshaji wake, bado inaendelea kuwahudumia wateja wake bila ya kubagua
dini, rangi wala kabila hivyo amewataka wateja wao kutambua kuwa Benki
hiyo ipo kwaajili ya kila mtu.
Alisema
kuanzishwa kwa huduma ya halal pesa kwa kushirikiana na mtandao wa simu
wa Vodacom kutasaidia watu wengi zaidi kufikiwa na huduma giyo ambayo
inafuata sheria za kiislamu.
Kwa
upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma za M-Pesa kutoka Vodacom,
Tulisindo Rashid alisema, halal pesa imelenga zaidi ya robo tatu ya
waislamu nchini Tanzania ambao kwa kupitia mfumo wa M-Pesa wataweza
kuweka fedha na kupata faida kihalali (bila ya riba).
Alisema
kwa muda mrefu waislamu wamekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za kuweka
fedha zinazfuata sheria za dini ya kiislamu ambapo huduma hiyo
itawezesha watumiaji wake kuweka fedha kwa njia rasmi ya halal pesa.
Alisema
Vodacom itaendelea kutoa ufumbuzi wa mambo mbalimbli ili kukidhi
mahitaji ya wateja wake katika mfumo wa kifedha kwa kutumia teknolojia
ya kidigitali yenye gharama nafuu na uwezo wa hali ya juu.
Aliongeza
kwa kusema, halal pesa ni huduma rahisi na ya kipekee inayoendana na
sheria za kiislamu ambayo imegawanyika katika mafungu mbalimbali.
Alifafanuwa
mafungu hayo ni pamoja na kuweka pesa binafsi, kwaajili ya kwenda hija,
watoto au kuweka pesa kwa muda mrefu kuanzia miezi 3 hadi 12.
Aidha,
alitoa wito kwa maimamu wa misikiti kufungua Akaunti kupitia halal pesa
ambapo msikiti utapewa namba maalum ya utambulisho (Code number)
itakayowawezesha waumini kuchangia michango ya msikiti hata kama hawapo
msikitini.
Alisisitiza
kuwa, huduma hiyo ni salama na kwamba inafuata misingi ya kiislamu kwa
kupata muongozo kutoka kwa wanazuoni wa kiislamu kuhusu masuala ya
kifedha.
Sheria ya
kiislamu imeharamisha riba na kuhalalisha biashara hivyo muislamu
anapofanya miamala ya kifedha huchunga mipaka ya kisheria na kujiepusha
na riba.
Kwa
huduma hii mpya ya halal pesa iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Amana
Bank na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom itamuwezesha muislamu
kuweka fedha Amana Bank na kuzitoa kwenye M-Pesa huku akiwa hakutani na
riba na badala yake atapata gawio la faida ambalo limeruhusiwa katika
sheria ya uislamu.
No comments:
Post a Comment