HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2019

POLEPOLE ATAKA MSHIKAMANO KWA WANA CCM WILAYA YA TANGA


Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole akizungumza wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Waze.

Sehemu ya wanachama wa CCM wilaya ya Tanga wakifuaatilia kwa umakini hotuba ya Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoani Tanga Ummy Mwalimu.

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole kulia akipokea tisheti ya umoja wetu ni ushindi wetu ya CCM kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge huyo katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba.
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole (wa pili kushoto), akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima ambaye ameshikilia fedha zilizochangishwa kwenye semina hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga, Meja Mstaafu Hamisi Mkoba.

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa anahesabu fedha zilizotolewa.

Na Mwandishi Wetu

WANACHAMA wa CCM Wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Hayo yalisemwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoani Tanga Ummy Mwalimu.

Alisema lazima kuwepo mshikamano ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha pia katika semina hiyo Katibu huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni 5.

Sambamba na uchangiaji huyo lakini Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .

No comments:

Post a Comment

Pages