Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kushoto), akiwa katika
picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB Ally
Laay (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,
Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), na Katibu wa Bunge Dk. Thomas
Kashilah (wa kwanza kulia), katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki
ya CRDB kwa jailli ya wateja na wadau wa benki hiyo.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela katika hafla ya futari
iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa jailli ya wateja na wadau wa benki
hiyo. Kulia ni Katibu wa Bunge Akt. Thomas Kashilah na kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Ally Laay.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Spika wa Bunge la Jumhuri ya
Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameipongeza Benki ya CRDB kwakuwa
mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za ujenzi wa taifa kupitia miradi ya
maendeleo kama vile ujenzi wa mradi wa ufuaji umeme wa Stiglers gogle na
mingine mingi.
Spika Ndugai aliyasema hayo wakati
wa futari maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dodoma.
“Tuna imani kubwa na Benki ya
CRDB. Siku zote nimekuwa nikisisita kuwa Benki hii ndio kioo halisi cha mabenki
yetu nchini. Mafanikio ya Benki ya CRDB yana akisi hali halisi ya uchumi wa
taifa na mtanzania mmoja mmoja. Hivyo basi, sisi kama Bunge tutaendelea kuwapa
kila ushirikiano unaohitajika. Watanzania wanajisikia fahari kuona Benki yao ya
kizalendo kiendelea kuimarika.”
Kwa niaba ya wageni waalikwa
ambao walihusisha Mawaziri, Wabunge na wateja wa benki ya CRDB, Mheshimiwa
Ndugai aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuundaa futari hiyo maalum jijini Dodoma.
“Tunawashukuru benki ya CRDB kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya
wateja wadau wake hapa Dodoma. Sisi watu wa Dodoma tunaona ufahari kwa kitendo
hiki kwani kinaonesha kuwa mnatujali, Ahsanteni sana” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela aliwashukuru wageni waalikwa kwa
kuhudhuria futari hiyo na kuwaahidi kuendelea kuboresha huduma za benki ya CRDB
ili kufikia matarajio yao. “Kipekee kabisa niwashukuru wageni wote mliofika
hapa leo.
Benki ya CRDB tumejiwekea utaratibu kila mwaka wa kushiriki katika
futari ili kuungana na ndugu zetu wa
kiislamu katika kuomba dua pamoja na kuomba yaliyo mema. Nichukue nafasi
kuwaahidi kuwa tutaendelea kuwa wabunifu huku tukiongeza utumiaji wa mifumo ya
kidijitali ili tuweze kuwapa huduma zitakazokidhi matarajio yenu. Sisi benki ya
CRDB tunandelea kuwaahidi huduma bora zaidi na ahadi yetu kwenu ni kuwa TUPO
TAYARI KUWAHUDUMIA”.
No comments:
Post a Comment