HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2019

Serikali ya Marekani Yazindua Mradi wa Lishe Endelevu ili Kukuza Lishe Nchini Tanzania

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Lishe Endelevu mkoani Rukwa. Kulia kwake mstari wa nyumba ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Andrew Karas. 


Rukwa, Tanzania

SERIKALI ya Marekani imezindua mradi wa Lishe Endelevu katika eneo la Kizitwe Manispaa ya Sumbawanga, mkoa wa Rukwa. Mradi huu mpya utasaidia kupunguza udumavu kwa watoto, kuongeza idadi ya watoto wanaopata milo yenye ubora, na kuboresha lishe kwa wanawake waliofikia umri wa kuzaa. 

Lishe Endelevu, inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na kutekelezwa na Save the Children, inaonesha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Marekani na Tanzania katika kuboresha maisha ya Watanzania. "Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania kwa kutambua kuwa watoto wenye afya ni viongozi wa baadae wa Tanzania. 

Lishe bora itawapa watoto wa Tanzania uwezo wa upeo wao katika afya, elimu, na uzalishaji wa kiuchumi, "alisema Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Andy Karas, wakati wa uzinduzi. 

Pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za lishe, Lishe Endelevu itasaidia shughuli za maji na usafi ili kusaidia lishe bora. Mradi huu pia utaongeza upatikanaji wa vyakula kwa kukuza mazao mengi yenye virutubisho, teknolojia ya kisasa, na ufugaji wa mifugo wadogo bora kwa afya. 

Kwa maelezo ya ziada kuhusu Lishe Endelevu, tembelea tovuti hii:
https://www.usaid.gov/documents/1860/lishe-endelevu-sustainable-nutrition

No comments:

Post a Comment

Pages