HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 29, 2019

Matukio Katika Picha Uwasilishaji Bajeti ya Wizara ya Nishati

  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Bungeni Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dastan Kitandula akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo leo Bungeni mara bada ya kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
 Mbunge wa Muleba Kusini Mhe. Charles Mwijage akichangia  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati   kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua akisisitiza jambo kwa  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),  Mhandisi Amos Maganga  nje ya viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma.
  Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi , Watendaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakifuatilia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
 Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi , Watendaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakifuatilia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa baadhi ya wageni waliofika Bungeni kwa lengo la kujifunza shughuli za Bunge.
Naibu  Waziri wa Nishati  Mhe. Subira Mgalu akisistiza kuhusu hatua  zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya umeme. (Picha na  Frank Mvungi- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Pages