Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya
Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.(Picha na Happiness Shayo).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George
H. Mkuchika (Mb) (hayupopichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi cheti cha ufanyakazi bora kwa
mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara ya Madini, Bi. Asteria Muhozya baada ya
ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St.
Gaspar jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb)
(kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili
kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya
Madini Bw. Issa Nchasi (kulia).
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb)
na Waziri wa
Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb) wakifurahia jambo baada ya ufunguzi mafunzo kwa
viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.Kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Idara ya
Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini
Bw. Issa Nchasi.
Na Happiness Shayo, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt
(Mst) George Mkuchika (Mb)
amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuwa waadilifu katika
utendaji kazi wao ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mhe. Mkuchika ametoa
wito huo alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika
ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
Mhe. Mkuchika amesema
kuwa, katika kulenga dira ya pamoja ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ni
lazima viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kufuata misingi ya maadili
kama inavyoelezwa katika Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma
za mwaka 2005.
Mhe. Mkuchika ameongeza
kuwa, kutozingatia viapo vya maadili ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Mkuchika
amewataka viongozi wa Wizara ya Madini kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza
kiapo cha uadillifu.
“Kiongozi unapaswa
kuwa mfano katika kutekeleza kiapo chako cha uadilifu, na kama utakuwa umesahau
kiapo chako, si vibaya ukaichukua nakala ya kiapo ofisini kwako na kujikumbusha
mara kwa mara,” Mhe. Mkuchika amesisitiza.
Mhe. Mkuchika amesema
kuwa ni vema watumishi wa Wizara ya Madini hasa wanaofanya shughuli zao katika
maeneo ya uchimbaji madini wawe waadilifu pia ili kuongeza tija na utendaji
kazi mzuri.
“Watumishi mlioko
kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji, muwe waadilifu na mtangulize
uzalendo wa nchi mnapotekeleza majukumu yenu” Mhe. Mkuchika amesema.
Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka
viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuepuka vitendo vya rushwa huku
akinukuu maneno ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hayati Koffi
Annan.
“Rushwa ni ugonjwa ambao unatafuna
taratibu na wenye kuleta madhara katika jamii. Unadhoofisha demokrasia na
utawala wa sheria, unaleta uvunjifu wa haki za binadamu, unaharibu hali ya
maisha, na kusababisha kuwepo kwa mauaji na mambo mengine yanayotishia usalama
wa binadamu” Mhe. Mkuchika amesema.
Katika tukio la ufunguzi wa mafunzo
hayo, Mhe. Mkuchika amekabidhi vyeti vya ufanyakazi bora kwa watumishi 12 wa
Wizara ya Madini.
Mafunzo ya viongozi wa
Wizara ya Madini yamefanyika lengo ikiwa ni kukumbushana stadi muhimu za kazi,
kuwajengea uwezo wa utendaji kazi na kuongeza ari ya utekelezaji wa majukumu
yao.
No comments:
Post a Comment