HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 19, 2019

MUFTI MKUU TANZANIA AITABIRIA MAKUBWA BENKI YA NMB

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw akimkaribisha Mufti  wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, wakati wa Futari iliyoandaliwa na NMB katika Hotel ya Serena. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Idd Badru.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuberi akisalimiana na wageni waliohudhuria wakati wa Futari iliyoandaliwa na NMB.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kabwe na Mkurugenzi wa ndni wa benki hiyo, Juma Kimori wakiwaongoza wageni kuchukua futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyodanyika kwenye Hoteli ya Flomi Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB katika Hoteli ya Flomi mkoani Morogoro.
Shekhe Mkuu Mkoa wa Mtwara, Nurdin Mangochi akiwa kwenye iftari iliyoandaliwa na Benki ya NMB.
 Mkurugenzi wa ndani wa Benki ya NMB Juma Kimori, akizungumza wakati futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB katika Hoteli ya Flomi mkoani Morogoro.


NA MWANDISHI WETU

MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, ameitabiria makubwa Benki ya NMB, kutokana na utamaduni chanya walionao wa kuijali, kuithamini na kuipa kipaumbele jamii chini ya mwamvuli wa kaulimbiu yao ya Karibu Yako.

Mufti Zubeir alitoa mtazamo huo wakati akizungumza na waaalikwa wa hafla ya pili ya benki ya NMB kufuturisha waumini wa Dini ya Kiislamu tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu 2019.

Ukiondoa Mufti Zubeir, hafla hiyo iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam, ikishirikisha waumini wa Kiislamu, wateja na waalikwa wengine, ilihudhuriwa pia na Sheikh Mkuu wa Mkoa, Alhad Mussa Salum na Meya wa Jiji, Issaya Mwita.

“Niwapongeze kwa uamuzi huu wa NMB kufuturisha waumini wa Kiislamu, hasa ukizingatia mnahudumia makundi mbalimbali wakiwemo Wakristo na wasio na dini. Hii inatoa tafsiri moja tu kuwa NMB inajali makundi na kada mbalimbali za jamii, jambo ambalo litawapa mafanikio.

Aliongeza ya kwamba walichofanya NMB ni jambo kubwa, linalojenga mahusiano makubwa baina ya Waislamu na wasio Waislamu, na kila mmoja kuitazama NMB kama taasisi inayojali makundi yote ya watu na kwa namna hiyo wanazivuta nyoyo za wengi kuona inafaya kazi kwa weledi.

“Mtu akiwa mwema kiasi hicho ama hata taasisi, Mwenyezi Mungu humlipa ama huilipa, hii maana yake ni kuwa kwa utamaduni huu, NMB itapata mafanikio makubwa kutokana na namna mnavyojali makundi mbalimbali ya jamii,” alisema Mufti Zubeir.

Aliitaka NMB kutoacha tamaduni ya kufungamanisha makundi kwa kufuturisha waumini wa Kiislamu na kuutaka uongozi kuufanya utamaduni huo kuwa wa kudumu ili pindi awamu moja ya uongozi inapomaliza muda wake, iache alama kwa jamii.

Awali akimkaribisha Mufti Zubeir, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw, alisema benki yake inajisikia furaha kuungana na Waislamu katika kutimiza moja ya nguzo muhimu za dini yao, huku akiahidi kuwa NMB itaendelea kusapoti na kushirikia na jamii.

Alisema tukio hilo ni la pili tangu kuanza kwa mfungo wa Ramadhani mwaka huu, baada ya kukutanisha, kufuturisha na kujadiliana kwa ufupi na Waislamu wa Jiji la Tanga na kwamba wamepanga kufuturisha katika miji kadhaa Tanzania Bara na Visiwani.

“Tukio kama hili leo linafanyika mjini Iringa, awali lilifanyika Tanga na sasa tunaelekea Zanzibar (Unguja na Pemba), na pia mikoa ya Mtwara, Mwanza na kwingineko kulingana na ratiba itakavyoturuhusu,” alisema Jonkergouw.

Akijibu wito wa Mufti Zubeir, aliyeomba muendelezo wa hafla za kufuturisha, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, alisema NMB itaendelea na utaratibu wa kufuturisha waumini wa Kiislamu na kwamba wamefanya hivyo mara nyingi na wataendelea

No comments:

Post a Comment

Pages