NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) Mkoa wa Mbeya umefanikiwa
kuwahakiki zaidi ya wastaafu 5000 ambao ni wanachama Mfuko huo tangu Rais John
Magufuli kutaka watataafu wote wahakikiwe.
Meneja wa Mfuko huo wa PSSF Mkoa wa Mbeya, Joseph
Fungo, alisema kuwa baada ya agizo la Rais Ofisi ya PSSSF mkoa ilianza
zoezi hilo mara moja na hadi kufikia mwezi machi mwaka idadi kubwa ya wastaafu walikuwa wamehakikiwa
na kuendelea kupata stahiki zao.
Fungo alisema kuwa idadi hiyo ya wanachama ni kutokana
jitihada ambazo zimesaidia kufanikisha zoezi hilo kwa kiasi kikubwa ni pamoja
na kuwa na utaratibu wa kuwatembelea na kuwahakiki
wastaafu hao majumbani kwao kwa wale ambao wanamatatizo mbalimbali yakiwemo ya ulemavu na
kuugua kwa muda mrefu.
‘’Zoezi la kuwatembelea watassfu ambao wanamatatizo
mbalimbali yakiwemo ya kuumwa na ulemavu majumbani kwao limekuwa msaada
mkubwa katika kufanikisha zoezi la
uhakiki’’alisema fungo.
Aidha,Fungo alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi la
uhakiki kumekuwa na kiwango kikubwa cha mwitikio wa wanachama,wastaafu na ndugu
kufika katika ofisi za PSSSF kwajili ya kupata huduma mbalimbali.
Alisema kwa siku wastani wa wateja zaidi ya 200
wamekuwa wakihudumiwa tangu mfuko huo
ulipo anzishwa baada ya mifuko mnne
kuunganishwa na kuwa mfuko mmoja.
Fungo alisema kutokana na mwitikio huo ofisi yake
imekuwa ikijitahidi kuwahudumia wateja
wakiwemo wastaafu kwa wakati ili kukidhi matakwa na mahitahi ya wateja.
Alisema katika zoezi hilo la uhakiki wa wastaafu
wamebaini mambo mbalimbali likiwemo suala la baadhi ya watu wa karibu kuendelea kunufaika na mafao
licha ya baadhi ya wastaafu kufariki dunia hatua ambayo imesaidia kuokoa
upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Mmoja wa wastaafu ambaye hakuwa tayari kutaja
jina,alisema kuwa tangu kuunganishwa kwa mifuko hiyo na kuwa mfuko
mmoja,amepongeza huduma bora zinazotolewa na watumishi wa PSSSF kwa mkoa wa
Mbeya.
‘’Niwe muwazi
huduma za mfuko wa PSSSF
zimeboreshwa kwa kuwa tangu nifike hapa nimehudumiwa kwa
wakati na hivyo niishukuru serikali kwa
kuunganisha mifuko hiyo na kuwa mfuko mmoja’’alisema
No comments:
Post a Comment