JESHI
la Polisi Kanda Maluum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa
Makosa ya Jinai (DCI), limeanza uchunguzi wa picha na video ya ngono
inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inayodhaniwa kuwa ya Askofu Josephat
Gwajima.
Kamanda Lazaro Mambosasa. |
Jana
Mei 7, kulianza kusambaa kwa video hiyo, kutoka kwa watu wasiojulikana kwenye
mitandao ya kijamii, zikidhaniwa kuwa ni za Askofu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima, akiwa anafanya ngono na mwanamke asiyefahamika.
Kwa
mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi zilizotolewa mchana mchana huu, jeshi hilo
linakiri wazi kuwa Askofu Josephat Gwajima sio mtuhumiwa wa picha hizo, bali ni muathirika na
kwamba jambo hilo linaweza kufanywa na mtu yeyote kwa lengo la kumchafua kwa
waumini wake.
“Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeanza uchunguzi wa picha na video za ngono mara
moja na linapenda kuwaarifu wananchi kuwa, Gwajima sio mtuhumiwa, bali
muathirika wa tukio hilo, kwani ni jambo linaloweza kufanywa n amt yeyote ili
kumchafulia kwa waumini wake,” ilisema taarifa hiyo.
Jeshi
hilo likaenda mbali katika taarifa yake hiyo iliyosainiwa na Kamanda Lazaro
Mambosasa, kwa kuonya kuwa wananchi waache tabia ya kusambaza video na picha
zinazokinzana na maadili, huku likiwataka waumini wa Askofu Gwajima kuwa
watulivu wakati uchunguzi wa kumbaini aliyefanya ukiendelea.
Baada
ya kusambaa kwa video hizo jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Lazaro Mambosasa, alitoa taarifa za jeshi lake kumtaka Gwajima aripoti
Makao Makuu ya Polisi, agizo alilopaswa kulitekeleza leo asubuhi, vinginevyo
angesakwa na kukamatwa popote.
“Tayari
Askofu Josephat Gwajima ameitwa Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho asubuhi (yaani
leo), akichelewa ataamatwa na tumemuita sababu hakuna aliyelalamika, lakini
tumeona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe Askofu ama mtu wa kwaida, ule
ni unyama,” alisema Kamanda Mambosasa.
Akizungumzia
tukio hilo leo, kwa waandishi wa habari, mbele ya maaskofu, wachungaji wa
makanisa mbalimbali, na waumini wake kanisani kwake Ubungo jijini Dar es
Salaam, Askofu Josephat Gwajima amezihusisha video hizo na kampeni chafu za kumnyamazisha
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, utakaofanyika nchini mwakani.
Mchungaji Gwajima. |
Gwajima
akaenda mbali kwa kulishangaa Jeshi la Polisi Kanda Maalum kumuita Polisi,
badala ya kuanza uchunguzi wa kumbaini aliyefanya kazi ya ‘kuedit’ picha na
kuchanganya matukio kisha kumuhusiha yeye kwa lengo la kumchafua.
“Nimeitwa
Polisi, yaaani niliyejurihiwa ajalini alafu niende Polisi, badala ya
walionijeruhi? Wamtafute huyu mtu wampate. Haiwezekani nichafuliwe mimi,
waliofanya hivyo wasikamatwe, ila akichafuliwa mtu fulani akichafuliwa muhusika
anapatikana haraka,” alisema huku akishangiliwa na waumini wake.
No comments:
Post a Comment