Askofu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima, akizungumambele ya maaskofu, wachungaji wa makanisa mbalimbali, na
waumini wake kanisani kwake Ubungo jijini Dar es Salaam leo, kuhusu video za udhalilishaji zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima, akizungumambele ya maaskofu, wachungaji wa makanisa mbalimbali, na
waumini wake kanisani kwake Ubungo jijini Dar es Salaam kuhusu video za udhalilishaji zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mke wa mchungaji Gwajima akizungumzia tukio hilo.
NA MWANDISHI WETU, DAR
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Gwajima, amejitokeza hadharani leo kuzikana
video za udhalilishaji zilizosambaa mitandaoni, akizitaja kama zao la picha za
kutengeneza na watu maalum ili kumchafua na kujaribu kumnyamazisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mbele ya maaskofu, wachungaji wa makanisa mbalimbali, na
waumini wake kanisani kwake Ubungo jijini Dar es Salaam, Gwajima amezihusisha
video hizo na kampeni chafu za kumnyamazisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na
Wabunge, utakaofanyika nchini mwakani.
“Kumekuwa
na mbinu chafu za watu, wanaofikiria tufanye hiki ili kumnyamazisha Gwajima,
sasa nawaambia hamuwezi kuninyamazisha. Ni mwanaume gani anaweza kufjamiiana na
mke ama mpenzi wake, huku akijirekodi mwenyewe, akatuma mwenyewe mitandaoni,”?
amehoji Gwajima.
Amebainisha
ya kwamba: “Ukiangalia video hizo, utagundua kwa mwili wa anayeshiriki vitendo
hivyo ni mwingine, kichwa cha mwingine, na hata mkono ni wa baunsa, tofauti na
wangu. Zilizotumika ni picha mgando kuunganisha na picha zingine ili
kufanikisha walichopanga.”
“Napunguzwa
nguvu kisa Uchaguzi Mkuu wa mwakani, wakijua kuwa wakati wa mchakato huo nitawatesa,
sasa hapa hapunguzwi mtu nguvu, waliofanya hivyo walichoithibitishia jamii tu
ni kuwa mimi ni mwanaume kamili, hawajanichafua. Hakuna mwanaume kamili
asiyeshiriki tendo hilo, ila hufanywa faragha,” akasema.
Aidha,
Gwajima amelishangaa Jeshi la Polisi kwa kitendo cha kumuita kuhojiwa, na
kwamba walichopaswa kufanya ni kuwasaka wachafuzi na kuwawajibisha kwa mujibu
wa Sheria za Makosa ya Mtandao na sio kumuita yeye aliyejeruhiwa.
“Nimeitwa
Polisi, yaaani niliyejurihiwa ajalini alafu niende Polisi, badala ya
walionijeruhi? Wamtafute huyu mtu anayemiliki akaunti ya Instagram kwa jina la Original,
wampate. Haiwezekani nichafuliwe mimi, waliofanya hivyo wasikamatwe, ila
akichafuliwa mtu fulani akichafuliwa muhusika anapatikana haraka.
“Nitasimama
imara na nitakuwa zaidi ya nilivyokuwa, nitasema zaidi ya uchaguzi uliopita. Nitapambana
na sitokufa, sifi, sitotekwa na sitoweza kuteswa na yetote,” akasma Gwajima,
ambaye aliambatana na mkewe, ambaye pia alizungumza na kusema anamjua na
kumuamini mumewe na haamini katika anayozushiwa.
Baada
ya kusambaa kwa video hizo jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Lazaro Mambosasa, alitoa taarifa za jeshi lake kumtaka Gwajima aripoti
Makao Makuu ya Polisi, agizo alilopaswa kulitekeleza leo asubuhi, vinginevyo
angesakwa na kukamatwa popote.
“Tayari
Askofu Gwajima ameitwa Polisi kwa ajili ya kuhojiwa na ataripoti kesho asubuhi (yaani
leo), akichelewa ataamatwa na tumemuita sababu hakuna aliyelalamika, lakini
tumeona ni kitendo cha ukiukwaji wa maadili, awe Askofu ama mtu wa kwaida, ule
ni unyama,” alisema Kamanda Mambosasa.
No comments:
Post a Comment