Meneja Kiongozi , Uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dodoma kuhusu hatua iliyofikiwa katika kulipa malimbikizo ya mafao
yao ambapo Takribani wastaafu
10,000/- wamelipwa.
Sehemu ya waandishi wa habari
wakifuatilia mkutano wa Meneja
Kiongozi , Uhusiano Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Eunice Chiume leo Jijini Dodoma ambapo
mfuko huo unaendelea kulipa mafao ya wanachama wake tangu ulipoanzishwa.
Meneja Kiongozi , Uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Eunice Chiume akitoa wito kwa wanachama wa mfuko
huo kuendelea kujitokeza katika Ofisi za mfuko huo kuhakiki taarifa zao ili
waweze kuendelea kupata huduma kwa mujibu wa sheria kuepuka usumbufu unaoweza
ukajitokeza.
Sehemu ya waandishi wa
habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja
Kiongozi , Uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma
(PSSSF) Eunice Chiume baada ya mkutano na waandishi ha oleo Jijini Dodoma.
(Picha
zote na Idara ya Habari MAELEZO).
Na Frank
Mvungi - MAELEZO
Wanachama elfu kumi wa Mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wamelipwa takribani Bilioni 880, 000/-
ikiwa ni malimbikizo ya Pensheni kwa wastaafu tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo mapema mwaka
jana.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dodoma Meneja Kiongozi, Uhusiano
wa mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema kuwa dhamira ya Mfuko huo ni kuhakikisha kuwa wanachama wake
wanaendelea kulipwa mafao yao kwa wakati kuendana na azma ya Serikali ya Awamu
ya Tano kuwafanya wastaafu wote kuishi maisha bora.
“Katika kipindi cha miezi 6 Mfuko
umeendelea kutoa huduma bora hali iliyowezesha wastaafu wetu zaidi124,000 kuendelea
kupata huduma zetu katika ofisi zetu za mikoani pamoja na Zanzibar” alisisitiza
Chiume.
Akifafanua amesema kuwa mfuko huo
una wanachama takribani 763,000 kote nchini na unaendelea kuimarisha mifumo ya
utoaji wa huduma bora kwa wanachama wake.
Mfuko huo umeendelea kutekeleza
dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kusimamia uwekezaji katika sekta hiyo
ikiwemo kiwanda cha viatu Karanga kilichopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kinachomilikiwa kwa ubia
na Jeshi la Magereza.
Eneo jingine ni uwekezaji katika
amana za Serikali, kiwanda cha Tangawizi kilichopo Same Mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wa zoezi la uhakiki wa
wanachama wa mfuko huo amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kati ya Desemba 2018
hadi Machi 2019 na ni endelevu.
Pia alitoa wito kwa wanachama wa
mfuko huo ambao wamestaafu kuhakiki taarifa zao kupitia ofisi za mfuko huo
zilizopo mikoani ili kuepuka usumbufu ikiwemo kusitishiwa pensheni.
Aliongeza kuwa dhamira ya kufanya
uhakiki huo ni kuwezesha mfuko kuhakikisha kuwa anayelipwa pensheni ni yule
anayestahili kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
Kwa upande wa watumishi wa mfuko
huo wameaswa kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa mfuko huo ili
kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora.
Mfuko wa PSSSF ni matokeo ya
kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili kuimarisha utoaji wa
huduma kwa wananchi hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya hifadhi ya Jamii hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment