Waziri
wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa
neon la ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji wa Uingereza nchini alipokutana
nao Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam
ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
NA MWANDISHI WETU
Serikali
imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji nchini ili
kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki yatakayowavutia kuwekeza nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakati akifungua mkutano wa wawekezaji wa Uingereza
waliopo nchini walipokutana kujadili masuala ya Uwekezaji uliofanyika Mei 29,
2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,
Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde, Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke
pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Biashara ya Uingereza Bw. Kalpesh Mehta,
viongozi wa makampuni ya uwekezaji nchini, pamoja na baadhi ya viongozi wa
Taasisi za Sekta ya Umma na Binafsi.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo, Waziri Kairuki alieleza lengo la kukutana na wawekezaji
kutoka Uingereza ni pamoja na kujadili masuala yote yanayowahusu wawekezaji kwa
kuzingatia changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzitatua ili
kuendelea kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya biashara na uwekezaji
nchini.
“Tumezingati
umuhimu wa wawekezaji nchini, hivyo tumekutana hii leo ili kusikiliza kero na
changamoto zinazowakabili ili kuona namna bora ya kuboresha mazingira na
kutambua fursa zilizopo nchini ili kuendelea kuwekeza nchini”, alisema Waziri
Kairuki.
Waziri
aliongezea kwamba, kwa kuzingatia kuwa mnamo mwezi Machi mwaka 2019 Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aliutangaza mwaka huu
kuwa ni mwaka wa uwekezaji alipokutana na waheshimiwa mabalozi wa nchi za nje
ambao wapo nchini ikiwa ni kiashiria cha kufungua mwaka mpya.
Aliongezea
kuwa, kwa kuzingatia mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo
ongezeko la ajira hivyo tunapaswa kuzingatia na kuboresha mazingira yatakayochochea
kuendelea kuchangia katika uzalishaji wa ajira nyingi nchini.
“Sekta
binafsi ndiyo kiini cha ukuaji wa uchumi kwa upande wa kuongeza ajira hivyo
tunatambua mchango huo ambapo hadi sasa wawekezaji wa uingereza wamechangia
katika ukuaji wa ajira kwa kuzalisha ajira laki tatu,”alisisitiza Waziri
Kairuki.
Kwa
upande wake Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya
Tanzania kwa kuona umuhimu wa kukutana pamoja kujadili masuala ya uwekezaji na
kuendelea kujadili namna ya kuwezesha wawekezaji kutoka uingereza kuendelea
kuwa wadau muhimu nchini na kuhakikisha nchi zote mbili zinanufaika.
“Ni
kweli tumeenedelea kuwekeza Tanzania kwa kuzingatia mazingira yaliyopo hivyo ni
vyema kukawa na maboresho zaidi katika mazingira hayo kwa kuendelea kutatua
changamoto zilizopo kwa sasa ili tuendelea kushirikiana pamoja,” alieleza
Balozi.Cooke
Aliongezea
kuwa nchi ya Uingereza imelenga kuwa kinara cha uwekezaji katika nchi za Afrika
hiyo ni wakati sahihi wa kuendelea kutumia fursa zilizopo barani humo ili
kufikia malengo.
“Ifikapo
mwaka 2022 Nchi yetu imeweka malengo ya kuwa wawekezaji bora barani Afrika
hivyo tunaendelea kushirikianana nchi za Afrika ili kuwa na nia moja na kuwa na
mahusiano yenye tija hasa katika masuala ya uwekezaji”,alisema Balozi Cooke.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na
Ajira Mhe. Anthony Mavunde alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuboresha
mazingira ya biashara ili kuchangia ongezeko la ajira kwa vijana wa Kitanzania
ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha
alifafanua kuwa, ili kuendelea kukuza ujuzi kwa vijana na kuondokana na
changamoto za ukosefu wa ajira Serikali itaendelea kulinda ajira za watanzania
na kuboresha mazingira ya sekta binafsi ambao ni wadau muhimu katika kuzalisha
ajira nchini.
No comments:
Post a Comment