Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Finland
nchini, Mhe. Pekka Hukka kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri
Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Pekka Hukka, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019.
*Akaribisha wawekezaji kwenye TEHAMA, uchakataji wa mazao ya kilimo na misitu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Mhe. Pekka Hukka, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Switzerland
nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni
jijini Dodoma, Mei 23, 2019.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Balozi wa Finland hapa
nchini, Mhe. Pekka Hukka na kumshukuru kwa jitihada za nchi hiyo
kuisadia Tanzania kuondokana na umaskini.
“Tunaishukuru
Serikali ya Finland kwa misaada ambayo imeendelea kuitoa kama njia ya
kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini pamoja
na kuongeza makusanyo ya mapato ili kukuza uchumi wa nchi yetu,”
amesema Waziri Mkuu.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) alipokutana na Balozi huyo anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu amemweleza balozi huyo kwamba Tanzania bado ina fursa za uwekezaji
na kwamba Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki na bora kwa
uwekezaji. “Sekta ambazo makampuni ya Finland yanaweza kuwekeza hapa
nchini ni pamoja na TEHAMA, nishati, usafiri, uchakataji wa mazao ya
kilimo na misitu,” amesema.
Waziri
Mkuu alimtakia heri Balozi Hukka ambaye anatarajiwa kuondoka nchini
mwishoni mwa mwezi huu kwenda Tunisia ambako ndiko kutakuwa na kituo
chake kipya cha kazi.
Kwa upande wake, Balozi
Hukka alisema ataondoka Tanzania akiwa na kumbukumbu nzuri ambazo
atazienzi na anataraji kukutana na Watanzania wengine ili aendelee
kukuza mahusiano yaliyokuwepo.
Alisema Serikali za Tanzania na Finland zilisaini mkataba wa programu iitwayo Forestry and Value Chain Programme (FORVAC)
ambao unalenga kuongeza faida za kiuchumi na kijamii kwa kupitia sekta
ya misitu pamoja na kupunguza ukataji wa miti. “Malengo hayo yatafikiwa
kwa kukuza mnyororo wa thamani kwenye sekta ya misitu pamoja na
kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, sheria na sera katika sekta ya
misitu,” alisema.
Finland inasaidia sekta ya misitu nchini Tanzania kupitia Programu ya Private Forestry Programme (PFP)
ambayo ililenga kuongeza mapato kwa wakazi wa vijijini katika
Halmashauri 10 za Njombe TC, Njombe DC, Makete, Ludewa, Kilombero,
Mufindi, Kilolo, Madaba, Mbinga na Nyasa) kwa kusaidia upandaji wa miti
na kuongeza thamani ya mazao ya misitu.
Programu
hiyo imesaidia kujenga uwezo kwa wahusika wote katika mnyororo wa
thamani wa biashara ya mazao ya misitu. Awamu ya kwanza ya programu hiyo
imesaidia kuongeza kipato cha familia zaidi ya 9,000 kwenye wilaya
hizo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Florence Mattli ambaye pia alienda kumuaga ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu alimweleza balozi huyo dhamira ya Serikali ya Tanzania ya
kudumisha ushirikiano na Uswisi na kusisitiza kwamba iko tayari kufanya
kazi na Balozi mpya wa Uswisi atakayekuja kwa manufaa ya pande zote
mbili.
“Ni
muhimu sana ushirikiano wa Tanzania na Uswisi ukadumishwa kwa
kuzingatia pia masuala ya biashara na uwekezaji hususan kwenye sekta za
afya, kilimo, elimu na teknolojia,” alisema Waziri Mkuu.
Alitumia
fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Uswisi kwa misaada ambayo imeendelea
kutolewa na nchi hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya
Tanzania za kuondoa umaskini hususan kwenye miradi ya afya, kilimo na
uwekezaji katika elimu na biashara kwa ajili ya kukuza uchumi.
Kwa upande wake,
Balozi Mattli alisema Serikali ya Uswisi imekuwa ikiunga mkono na
kusaidia jitihada za kukuza uwazi na uwajibikaji kwa watendaji wa
Serikali na wale wasiokuwa wa Serikali kuzingatia mazingira ya kitaasisi
na kijamii yanayopiga vita masuala ya rushwa.
“Msaada
huo wa kupambana na rushwa umechangia kuimarisha ufanisi wa uendeshaji
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kukuza uelewa
wa kijamii kuhusu masuala ya rushwa,” alisema.
Alisema
mwaka 2018, Serikali ya Uswisi ilitoa dola za Marekani milioni 24
kusaidia Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Ajira Tanzania, ambao ulianza
kutekelezwa Agosti Mosi, 2018 kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia.
“Mpango
huo unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa vitendo na
kuimarisha mafunzo ya ufundi nchini. Hivyo, mpango huo umechangia
kuboresha matarajio ya vijana kwa kuwapatia ujuzi katika kazi na ubunifu
unaochangia kuondokana na suala la ukosefu wa ajira,” alisema.
Alisema
Serikali ya Uswisi inasaidia maendeleo ya vijana kupitia Mpango wa
Ajira ya Vijana (OYE) ambao unalenga kuimarisha maisha ya vijana wa
kiume na wa kike kwa kuwafundisha fursa za ajira katika sekta za
biashara, kilimo, nishati mbadala, usafi wa mazingira na kuboresha
ujuzi.
No comments:
Post a Comment