Wito umetolewa kwa Serikali na watunga sera kuakikisha wanapitia upya na kufanya mabadiliko katika sheria ya usalama barabarani hili kuweza kudhibiti ajali zinazotokana na uzembe wa watu kwa makusudi.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Mary Richard alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani kwa umoja wa mataifa.
"Sheria hiyo kwa sasa ina mapungufu mengi kiasi mtu akikutwa na kosa adhabu zake ni za kawaida na makosa mengi yamebainishwa katika kanuni badal aya sheria yenyewe ametaja sheria hii inamtaja mtu aliyekaa siti ya mbele na Dereva ndio wanapaswa kufunga mkanda wakati kanuni inataja abiria wote wafunge mkanda jambo ambalo lina ukakasi kidogo"amesema Mary.
Mary ametaja kuwa sheria hii ya Sasa inaseama Dereva wa pikipiki ndio anapswa kuvaa kofia ngumu peke yake wakati sasa jeshi la Polisi ketengo usalama barabarani wameweka kanuni Dereva na abairia ndio wanapaswa kuvaa kofia hivyo ni bora vitu vyote hivi vingewekwa kwenye sheria hivyo tunaomba mamlaka zinazousika pamoja na Wizara ya Mambo ya ndani waangalie utaratibu wa kubadilisha sheria hii.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma , Fatma Toufiq amesema kuwa ajali za barabarani zinaepikika kama watanzania wote wataweza kufata sheria na kuwa makini pindi wanapoendesha vyombo vya moto.
Amesema kuwa yeye kama mbunge anayeshiriki katika kutunga sheria atasimama kidete kuhakikisha sheria hii mpya ya usalama barabarani inapatikana hli tuweze kupunguza takwimu za ajali na walemavu wakudumu wanaotokana na ajali za barabarani
Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Mary Richard, akizungumza na waandishi juu wiki ya usalama barabarani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Fatma Toufiq, akieleza ushuhuda wake kwa waandishi wa habari juu ya ajali ilivyoweza kumletea cahangamoto ya utendaji katika kazi
Mratibu wa Usalama Barabarani kutoka shirika la umoja wa Mataifa la WHO, Mary Kessy, akaizungumza mpango wa shirika lake katika kudhibiti usalama barabarani
Muwakilishi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani(RSA), John Seka, akieleza namna tasisi yao ilivyojipanga na inavyoshirikiana na jeshi la Polisi kutoa taharifa za watu wanaokiuka sheria za Usalama Barabarani.
Sehemu ya Waandishi wa habari walioshiriki Mkutano juu ya Masuala ya Usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Tamwa.
No comments:
Post a Comment