Bondia Muingereza Anthony Joshua, akiwa ameangukia kamba baada ya konde zito kutoka kwa mpinzani wake Andy Ruiz Jr wa Mexico, wakati wa pambano masumbwi usiku wa kuamkia leo. (Picha na Daily Mail).
Bondia Ruiz Jr akiwa na wapambe wake na mikanda aliyotwaa wakishangilia ushindi dhidi ya Joshua.
Joshua chali aisee.
Mwamuzi akimuangalia Joshua baada ya kutupwa sakafuni raundi ya tatu.
Mwamuzi akimuangalia Joshua baada ya kutupwa sakafuni raundi ya tatu.
Ruiz Jr akirushiana makonde na Joshua wakati wa pambano lao.
Ruiz Jr akiwa amekalishwa na Joshua kunako raundi ya tatu.
NEW YORK, MAREKANI
BONDIA machachari wa kimataifa wa England, Anthony
Joshua, amepoteza mikanda yake ya ubingwa wa Dunia, baada ya kukubali kipigo
cha raundi ya saba kutoka kwa Mmexico Andy Ruiz Jr, kwenye Ukumbi wa Madison
Square Garden, New York.
Pambano hilo la uzaji wa juu, limeunguruma usiku wa
Jumamosi kuamkia Jumapili jijini New York, Marekani, ambako kipigo kimemfanya
Joshua maarufu kwa la AJ (ambalo ni kifupisho cha majina yake), kupoteza
mikanda mitatu ya Dunia ya WBA, WBO na IBF.
Anthony Joshua alilianza pambano hilo taratibu na
kuibua hofu ya kutimia kwa tambo zake za kutopoteza pambano hilo alizokuwa
akizitoa kuelekea mtifuano huo na mwanzo wake huo haukushangaza kumuona
akilambishwa sakafu kunako raundi ya tatu, ingawa alimudu kuendelea naye
kumkalisha Ruiz Jr.
Kwa ushindi huo, Ruiz Jr – ‘bonge mwenye mwili
nyumba na minyama uzembe ya kumwaga,’ ameweka rekodi ya kwa bondia wa kwanza wa
Mexico kuwa bingwa wa Dunia wa masumbwi ya uzani wa juu. Mwamuzi wa pambano la
jana usiku, alikuwa ni Mike Griffin.
Daily Mail
No comments:
Post a Comment