Mwenyekiti
wa mashindano ‘Kabati Challenge Cup 2019’, Gerald Malekela, akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo mkoani Iringa ambapo jumla ya timu 44 zitashiriki.
Na Denis Mlowe, Iringa
MASHINDANO ya kugombea kombe linaloandaliwa na mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya CCM, Rita Kabati yanayojulikana kwa
jina la ‘Kabati Challenge Cup 2019’ yamezinduliwa rasmi kwa kuzikutanisha timu
za Kitwiru Fc na Black Eagle katika mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya Msingi
Ipogoro.
Katika mchezo huo ambao uliingia dosari katika dk ya 90
baada ya mashabiki wa Black Eagle kuingia uwanjani kugomea goli la tatu
lilofungwa kwa njia ya penati na timu ya soka ya Kitwiru hali iliyolazimika
refa wa mchezo huo kumaliza na kupewa ushindi timu ya Kitwiru na Black Eagle
kuondolewa rasmi katika mashindano hayo yanayofanyika kwa njia ya mtoano.
Katika mchezo huo magoli ya Kitwiru mawili yalifungwa
na Joseph Mlua dk. 6 na dk 50 na goli la tatu lilifungwa na George Luvanda
katika dk 90 huku magoli ya Black Eagle yalifungwa na Jackson Mhavile dk 25 na
Bony Kilave wa Kitwiru alijifunga katika dk. 75. na kuipatia timu ya soka ya
Black Eagle goli la pili.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, Mwenyekiti
wa mashindano hayo, Gerald Malekela alisema kuwa jumla ya timu 44 za mkoani Iringa zitashiriki
mashindano ya Ritta Kabati Challenge awamu ya tatu 2019 katika viwanja
mbalimbali ya mpira wa miguu mkoani Iringa kwa kuzishilikisha timu za wilata ya
Iringa, Iringa vijijini na Mufindi.
“Kwa mara ya kwanza tumepata timu nyingi kutoka katika
halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini kwa kujitokeza timu kumi na moja hiyo
inaonyesha jinsi gani kila kukicha mashindano haya yanazidi kuwa na mvuto na
ushindani unaongezeka” alisema Malekela
Malekela alisema msimu huu mashindano yatakuwa bora
kuliko misimu iliyopita kwa kuwa kamati imejipanga kuhakikisha wanatengeneza
kitu kilicho bora na kuongeza thamani ya mashindano na kuweka alama ya kuigwa
kwa wapenda michezo hasa mchezo huu wa mpira wa miguu.
Malekela aliongeza kuwa lengo la mashindano ni kuibua
vipaji vya vijana mkoani wa Iringa, lakini pia kutengeneza ajira kwao, sambamba
na kutengeneza kizazi chenye afya bora na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.
Aidha alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa yakikumbwa
na changamoto ya ubovu na uhaba wa viwanja vya mpira wa miguu,hivyo tunaiomba
serikali kuhakikisha wanatusaidia kuboresha viwanja hivyo.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Iringa,(IRFA)
Dk. Ally Ngala alisema kuwa kuwa
mbunge huyo ameonyesha jitihada
kubwa katika kuendeleza soka mjini Iringa na kumuomba kuendelea
zaidi kusaidia soka Iringa.
Ngala alisema
mashindano hayo yameleta chachu kubwa ya soka katika mkoa wa Iringa
ambapo vijana wengi wamehamasika na kuonyesha
uwezo wa hali ya juu katika soka
na kuwa lazima kuweka mkakati wa kudumu wa
kuendeleza vijana hao kisoka
No comments:
Post a Comment