HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

MEJA JENERALI KAPINGA MGENI RASMI PAMBANO LA NGUMI JUNI 7 JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mafunzo na Utendeji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga ambaye atakuwa mgeni rasmi katika pambano la ngumi Juni 7, 2019 katika ukumbi wa 361 Mwenge jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani JWTZ).

Na Selemani Semunyu

Mkuu wa Mafunzo na Utendaji kivita wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Afred Kapinga anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika pambano la Ngumi za Kulipwa na Ngumi za wazi linalotarajiwa kufanyika Juni Saba katika  Klabu ya Jeshi ya 361 Mwenge  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mmoja wa Waratibu wa Pambano hilo lisilola ubingwa Beatrice Ntahona alisema   Maandalizi yote yamekamilika ikiwemo hali za Mabondia na kinachosubiriwa ni mchezo mzuri huku mashabiki wakiangalia mpambano mzuri.

Tumemualika Meja Jenerali Kapinga kutoja JWTZ kwanza ndie msimamizi mkuu wa masuala ya Michezo Jeshini na Jeshi limekuwa na Mchango mkubwa katika kuendeleza Michezo hapa nchini katika nyanja zote ikiwemo  katika Ngumi.” Alisema Beatrice.

Aliongeza kuwa   mbali na Mgeni rasmi lakini kwa Upande wa Maandalizi yote yamekalika na tunataraji kupata watu wengi wapenzi wa Ngumi ambao walikuwa wakishindwa kuhudhuria kutokana na mazingira ya kumbi lakini katika ukumbi huu  usalama ni wa uhakika wa mashabiki na Mali zao.

“ Tumeandaa Pambano kwa Kuwashirikisha wa Ngumi za Wazi ili kutimiza Malengo ya Waaandaaji ambayo ni kuamsha hisia na Mashabiki wa Ngumi na kurejesha upinzani uliokuwa ukijitokeza wakati wa miaka ya Nyuma katika ngumi’  Alisema Beatrice.

Pia Aliongeza kuwa Anawashukuru kamisheni ya Ngumi za  za Kulipwa nchini kutokanana kuidhinisha pambano na pia kutoa ushirikiano ikiwemo kuandaa waamuzi watakaohakikisha mchezo huo unafanyika kwa kufuata sheria zote za  Mchezo huo.

Aidha alisema kama ilivyokuwa kwa Kamaisheni ya Ngumi za Kulipwa na Shirikisho la Ngumi za Wazi OBFT nako wamebariki kuchezwa kwa pamabno hilo kutokan na kushirikisha Wachezaji wa Ngumi za wazi wenye Upinzani wa Jadi Ngome  na Jeshi la Kujenga Taifa JKT.

Miongozi mwa Wachezaji wanaotaraji kuonyesha mchezo mzuri  katika Ngumi za Wazi  ni  Selemani Kidunda ambaye ni Nahodha kwa  Ngome,Hafidh Mlawa  wa JKT , Ismail Galiatano  wa Ngome, Swahibu Ramadhani  wa JKT Sambamba na Steven Anastaz wa JKT ambao wote wameitwa timu ya Taifa ya Ngumi..

Kwa upande wa ngumi za kulipwa Nasib Ramadhani atapambana na Bondia ambaye hajawahi kupigwa kwa KO Mohamed  Kashinde  wakati  Baina  Mazola na  Kudura Tamimu kutoka Morogoro huku   Bingwa wa  Ngumi na Mateke Jeremia Joshua atacheza na Hashim Masungo wakati kaisi Ally atamenyana na Bakari Mohamed.

No comments:

Post a Comment

Pages