HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

R.I.P. ‘MSHIKA BUNDUKI’ JOSE ANTONIO REYES

Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mchezaji wa Arsenal, Jose Antonio Reyes, kuingia na kutoka katika Kanisa la Santa Maria, mjini Utrera, Hispania leo Jumatatu asubuhi kwa ajili ya ibada maalum. 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mchezaji wa Arsenal, Jose Antonio Reyes, kuingia katika Kanisa la Santa Maria, mjini Utrera, Hispania leo Jumatatu asubuhi kwa ajili ya ibada maalum. 
Mwili wa Jose Antonio Reyes ukiwasili kanisani.
Ibada ya kumuombea Jose Antonio Reyes ikiendelea.
Picha tofauti za waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mchezaji wa Arsenal, Jose Antonio Reyes, kuingia na kutoka katika Kanisa la Santa Maria, mjini Utrera, Hispania leo Jumatatu asubuhi kwa ajili ya sala maalum. 

Reyes na binamu yake Jonathaan, walifariki kwa ajali ya gari aina ya Mercedes Brabus S550V, iliyokuwa katika mwendokasi wa kilomita 147 kwa saa, ajali ikitokea jirani na mji wa Alcala de Guadaira, karibu na Seville.

Ukiondoa Arsenal ya England, timu zingine alizowahi kuchezea Reyes aliyefariki wikiendi iliyopita akiwa na miaka 35 ni Sevilla, Real Madrid, Atletico de Madrid, Benfica, Espanyol, Cordoba, Xinjiang Tianshan Leopard F.C. ya China na Extremadura UD aliyokuwa akicheza hadi sasa.

Reyes ameacha mke Noelia Lopez, aliyekuwa amezaa naye watoto wawili wa kike - Noelia na Triana. Pia ameacha mtoto wa kiume anayeitwa Jose Antonio Jr, aliyezaa na mpenzi wake wa zamani kabla hajamuoa Noelia.
Reyes anazikwa leo jioni.

No comments:

Post a Comment

Pages