Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberates Sabas, akikagua mradi wa ujenzi wa Nyumba za Askari Polisi uliofadhiliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, katika eneo la Ikwiriri, Mkoa wa Kipolisi Rufiji na kulidhishwa na maendeleo mazuri ya ujenzi huo.
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo ya Jeshi la
Polisi CP Liberates Sabas, akizungumza na wanakijiji cha Rungungu baada
ya kuwatembelea na kutaka kujua maendelea yao na Usalama wa Kijiji
hicho, hatua hiyo ya kuwatembelea wanakijiji hao kamishna CP Sabas
huifanya mara kwa mara kwasababu ya kijiji hicho ndicho kilikuwa makazi
makuu ya wahalifu pamoja na eneo walilokuwa wakifanyia mafunzo yao kabla
ya kutimiza azima zao katika kipindi cha miaka ya 2016 na 2017.
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo ya Jeshi la
Polisi CP Liberates Sabas, akiwa katika picha ya pamoja na askari wa
kikosi maalum cha kupambana na wahalifu katika pori la Rungungu liliopo
Kijiji cha Rungungu katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji baada ya kumaliza
kufanya Operesheni maeneo hayo. (PICHA NA JESHI LA POLISI).
No comments:
Post a Comment