Mratibu wa Onyesho
la muziki lijulikanalo kama ‘The Eid Al Faris 2019",
Antonio Nugaz, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 6, 2019, wakati wa kutambulisha onyesho hilo.
Mkurugenzi wa Van Mo Company Ltd, Abdul Mohamed, akifafanua jambo wakati wa kutambulisha kwa waandishi wa habari onyesho la "Eid Al Faris 2019" litakalofanyika Juni 7, 2019 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Van Mo Company Ltd, Abdul Mohamed, akifafanua jambo.
Sheikh Masoud Feruzi kutoka Nasaha Crew akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa kundi lao katika onyesho hilo.
Msanii wa Komedi kutoka nchini Kenya, Sammy Kioko, ambaye naye atakuwepo katika onyesho hilo.
Msanii wa Komedi kutoka Kenya, Nasra Yusuph, akizungumzia onyesho hilo.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Kitanzania ya Van Mo Company Ltd ya jijini Dar es Salaam, imetambulisha Onyesho
kubwa na la aina yake la muziki lijulikanalo kama ‘The Eid Al Faris 2019,
linalofanyika Ijumaa hii Juni 7, kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mratibu wa onyesho, Antonio Nugaz, Eid Al Faris ni jukwaa la aina
yake kuwahi kufanyika nchini Tanzania, litakalojumuisha burudani mbalimbali,
ikiwemo vichekesho, nyimbo za dini (Qaswida), sambamba na chakula cha usiku.
Nugaz
alibainisha ya kwamba, matamasha kama hayo ni utamaduni uliozoeleka sana
miongoni mwa Waislamu na jamii za watu wa Mwambao, hususani katika kipindi cha
Sikukuu ya Eid el Fitr, huku akiwataka Watanzani kujitokeza kushuhudia burudani
hizo ndani ya Eid Al Faris.
Alifafanua
ya kuwa, Eid Al Faris litapambwa na burudani kutoka kwa Wakali wa Qaswida wa
Kundi la Nasaha, huku Sitti and The Band, ikialikwa kutumbuiza katika mahadhi,
mirindimo na maudhuhi ya Qaswida.
“Pia
kutakuwa na vichekesho kutoka kwa mastaa wa Komedi kama vile Nasra na Sammy
Kioko kutoka Nairobi, Kenya, ambako viingilio vitakuwa ni Sh. 50,000 (bila
chakula), Sh. 100,000 (pamoja na chakula) na Sh. 130,00 (sambamba na huduma za
ziada za ki-VIP).
Naye
Mkurugenzi wa Van Mo Company Ltd, Abdul Mohamed, alisema Eid Al Faris 2019 limeratibiwa
na kampuni yake hiyo, huku likiwezeshwa na Kampuni za GSM Africa, Superdoll,
VIMTO na ASAS Group, huku Clouds Fm (wakiwa ndio Official Radio partner) na
Azam TV (official broadcaster and TV patners).
No comments:
Post a Comment