HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2019

TradeMark East Africa yaimwagia TPSF Bilioni 2.7/-

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, akizungumza wakati wa kupokea msaada wa  dola za Marekani, USD 1,190,000, sawa na Shilingi Biloni 2.7 za Tanzania,  toka Taasisi ya Trade Mark East Africa, Tawi la Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 3, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) tawi la Tanzania, John Ulanga. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (kulia), akizungumza wakati wa kupokea msaada wa  dola za Marekani, USD 1,190,000, sawa na Shilingi Biloni 2.7 za Tanzania,  toka Taasisi ya Trade Mark East Africa, Tawi la Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) tawi la Tanzania, John Ulanga, akizungumza kuhusu taasisi yake imetoa dola za Marekani, USD 1,190,000, sawa na Shilingi Biloni 2.7 za Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) tawi la Tanzania, John Ulanga (kulia),  na  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, (kushoto), wakisaini mkataba ambapo  Taasisi ya Trade Mark East Africa, imetoa dola za Marekani, USD 1,190,000, sawa na Shilingi Biloni 2.7 za Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. Nyuma ni maofisa wa TMEA na TPSF wakishuhudia.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) tawi la Tanzania, John Ulanga, ( wa pili kulia)  na  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (wa pili kushoto) wakibadilishana makbrasha baada ya taasisi ya Trade Mark East Africa, kutoa dola za Marekani, USD 1,190,000, sawa na Shilingi Biloni 2.7 za Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. 


Na Mwandishi Wetu

TAASISI  ya Trade Mark East Africa (TMEA) tawi la Tanzania, imetoa dola za Marekani, 1,190,000, sawa na Shilingi Bilioni 2.7- za Tanzania, kwa Taasisi ya  Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.

Mkataba wa msaada huo, umesainiwa jijini Dar es Salaam leo Juni 3, 2019 kati ya Mkurugenzi Mkazi wa TIMEA hapa Tanzania, John Ulanga na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye,  kwenye ofisi za TPSF, Masaki, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia msaada huo, Ulanga amesema TMEA imeamua kuifadhili TPSF katika eneo la majadiliano na serikali katika kuboresha mazingira ya kufanyabiashara Tanzania, kufuatia Tanzania kuwa ndio nchi pekee yenye fursa nyingi zaidi za kibiashara kati ya nchi zote za Afrika Mashariki kufuatia kupokana na nchi nane zisizo na bahari, hivyo kuitegemea Tanzania kupitisha mizigo yake.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye, ameishukuru  TradeMark kwa msaada huo, na kuelezea umekuja wakati muafaka wa majadiliano na serikali, yakiendelea.

TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, linalohusika na maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara.

TMEA ni taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.

TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko, kuboresha mazingira ya biashara, kuboresha biashara ya ushindani.

Mchango mwingine wa TMEA, ni kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.

Aidha, TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.

Kwa upande mwingine, kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www.trademarkea.com
 

No comments:

Post a Comment

Pages