Washtakiwa waliochoma kituo cha Polisi wakiingia mahakamani
Wakili wa warufani Prof. Abdallah Safari, akizungumza na ndugu wa warufani hao nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Na Janeth Jovin
RUFAA
dhidi ya washtakiwa watatu kati ya wanane waliohukumiwa kifungo cha
maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha
polisi bunju imeshindwa kuanza kusikilizwa kufuatia majalada ya warufani
hao kuchanganywa.
Hali hiyo
imetokea leo Juni 13,2019 baada ya wakili wa Serikali, Sadah Mohamed
kuieleza mbele ya Naibu msajili wa Mahakama Kuu, Crisencia Kisongo kuwa,
rufaa hiyo leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mwenendo wa kesi
(proceedings) alionao siyo za mrufani aliyekuwa mahakamani hapo, bali
anayo ya mrufani Abrahamu Minga.
Alidai
wanaomba muongozo wa mahakama ili kufahamu nini kifanyike, rufaa
iliyoko mbele yako ni ya mrufani Konzo ambayo hajaipata na si ya mrufani
Minga aliyonayo.
Wakili
wa warufani hao Profesa Abdallah Safari alidai kuwa samasi (hati ya
wito) aliyonayo yeye ni ya washtakiwa watatu ambao ni, Yusuph Sungu
maarufu kama Mayuku ambae leo hakuwepo mahakamani, Juma Konzo na
Abrahamu Minga ambapo maelekezo ya warufani hao.
Baada ya maelezo hayo rufani hiyo imeahirishwa hadi Juni 17,2019
Februari
23, mwaka huu, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia wakili wake
Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwahukumu kifungo cha maisha washtakiwa
wanane baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha
Polisi cha Bunju A ambapo 10 waliachiwa huru.
Waliohukumiwa
ni Yusuph Sugu (40), Juma Kozo (32), Rashid Liwima (29), Baraka Nkoko
(23), Abuu Issa (36), Abraham Mninga (23), Veronica Ephraem (32) na
Ramadhan Said (22).
Walioachiwa
huru ni Mrisho Majaliwa (30), Hamis Ndege (37), Seleman Gwae (33),
Menge’nya Anthony (28), Rehema Hussein (32) Rajabu Ally (25), Ally
Athuman (24), Amina Matipwili (33), Gubila Temba (51) na Mariam Honza
(44).
Walikuwa
wanakabiliwa na makosa sita likiwamo la kuchoma kituo hicho moto ambapo
wanadaiwa Julai 10, 2015. Walichoma kituo cha polisi ambacho ni mali ya
umma jambo ambalo ni kosa la kisheria.
No comments:
Post a Comment