Na Talib Ussi, Zanzibar
Chama cha ACT-Wazalendo
kinatarajia kufanya Uchaguzi wake katika ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho
kwa ajili ya kupata safu mpya ya uongozi ya kujipanga kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi mkuu
mwakani.
Akizungumza na
waandishi wa habari Visiwani hapa Ofisa wa Kampeni na Chaguzi, Muhene Said Rashid, alisema chaguzi hizo zitaanza rasmin
mwezi ujao.
Alisema chama chao kina
aina mbili ya chaguzi ambapo moja ni ile katika ngazi ya Tawi, Jimbo, Mkoa na
Taifa pamoja na chaguzi za Ngome zake.
Alifahamisha kuwa chama
hicho kina ngome tatu ambazo ni Ngome ya Wanawake, Ngome ya Vijana na Ngome ya
Wazee.
Alieleza kuwa chaguzi
zote mbili zitaanza kwa kuchukua fomu na kurejesha kuazia tarehe 9-15
Agosti mwaka huu kwa kuogombea nafasi za
matawi na tarehe 19-25 August ni uchaguzi
wa matawi.
Pia alieleza kuwa
kuazia Tarehe 30 August hadi 05 September
2019 uchaguzi ngazi za Jimbo na Uchaguzi wa ngazi ya Mkoa iinatarajiwa
kufanyika tarehe 10 hadi 15 September mwaka huu.
“Baada ya kukamilika
chaguzi hizo awali baadae kamati kuu itakaa na kutoa taarifa ya chaguzi ngome
pamoja na Uchaguzi mkuu ndani ya chama ambao utakamilika mwaka huu” alieleza
Muhene.
Ikumbukwe chama hicho
kilifanya uchaguzi wake wa mwanzo mwaka 2014 na kwa mujibu wa Muhene chama
hicho kinalazimika kufanya uchaguzi ili
kutimiza matakwa ya sheria za vyama vya siasa nchini.
No comments:
Post a Comment