Mwenyekiti wa Kituo cha Magnet Youth Sports, Tuntufye Mwambusi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu timu nne zitakazokwenda Norway na Sweden kushiriki mashindano ya vijana wenye miaka 11, 12 na 15 yatakayofanyika Julai 14-21. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Cornel Barnabas na kulia ni Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo. (Picha na Francis Dande).
TIMU nne za kituo cha Magnet Youth Sports, zinatarajia
kuiwakilisha Tanzania katika michezo inayotarajia kuchezwa katika nchi za
Norway na Sweden.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kituo hicho, Tuntufye
Mwambusi, mashindano hayo yanatarajia kuanza Julai 14-21 yakishirikisha vijana
wenye miaka 11, 12 na 15.
Mwambusi, alisema katika mashindano hayo, kituo
hicho kitaungana na Sekondari ya St. Patrick ya jijini Dar es Salaam.
“Tunakwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano
hayo, ambayo yanakuwa na timu hadi 3,000, tutafanya vizuri katika mashindano
hayo,” alisema Mwambusi.
Alitumia fursa hiyo, kuwaomba wadau na serikali
kuboresha zaidi michezo kwa kukuza na kuendeleza vijana, ambao ndio tegemeo la
timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Cornel Barnabas, alisema hivi sasa mkazo wao
wameuelekeza zaidi kwenye soka la vijana, ambalo ndio nguzo ya michezo.
No comments:
Post a Comment