Meneja Mwandamizi Uhusiano Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha akizungumza wakati wa mkutano
wa NMB na Wafanyabiashara (NMB Business Club) mjini Babati Mkoani wa Manyara.
Mfanyabiashara
Ophii Urasa akizungumza
wakati wa mkutano wa NMB(NMB Business Club) na wafanyabiashara
wanaonufaika na mikopo ya benki hiyo kwa wilaya za Babati, Hanang na
Mbulu mkoani Manyara.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa jimbo
la Babati Mjini,Pauline Gekul amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya
kuendeleza biashara zao baada ya serikali kuondoa mlolongo wa tozo mbalimbali
zilizokua zikitozwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kabla ya kufungua biashara.
Akizungumza
katika mkutano uliondaliwa na benki ya NMB kwa wafanyabiashara mkoani
Manyara (NMB Business Club) mjini Babati alisema waache kulalamikia mazingira ya
biashara kwani katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 serikali imesikiliza
kilio chao.
“Nawapongeza
NMB kuwa na utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara na kuwapa maarifa ya
mikopo na kukuza biashara zenu,naamini mtaendelea kutoa mikpo zaidi kwa
wananchi wangu ili waweze kujiletea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za
kiuchumi,”alisema Gekul
Meneja Mwandamizi
wa NMB Wogofya Mfalamagoha alisema NMB ipo tayari kuwahudumia wafanyabiashara
wa ngazi zote kutokana na mtandao uliosambaa nchini nzima ikiwa na matawi zaidi
ya 228 na mawakala 6,800.
“NMB ina wafanyabiashara zaidi ya 200,000 nchi nzima ambao
wamechukua mikopo yenye thamani ya Sh 600 bilioni,mtakubaliana name kuwa
mikutano ya wafanyabiashara ambayo tunaifanya kuwaelimisha mambo ya biashara
imekua na tija kwetu sote,”alisema
Mfalamagoha.
Aliwataka
wafanyabiashara kutokutanguliza dhamana zao wanapotaka kuchukua mikopo bali
wazo la biashara ambalo linaweza kuwaletea faida kwani benki haipendi kuuza
dhamana za wateja baada ya kushindwa kurejesha mikopo waliyochukua.
Alisema shughuli
za wafanyabiashara wadogo na kati ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi
ikizingatiwa kuwa uchumi kwa ujumla wake unategemea mafanikio ya shughuli za
kibiashara zinazofanywa na wafanyabiashara wadogo na kati nchini na duniani.
“Lengo la
kukutana nanyi ni kuhakikisha mnakuza mitaji yenu, kutoa ajira kwa watanzania
wengi zaidi na kuchangia uchumi kupitia ulipaji wa kodi na kwamba NMB
imejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora kwa jamii ya wafanyabiashara katika
makundi yao,”alisema Mfalamagoha
Mwenyekiti wa
wafanyabiashara(NMB Business Club) Mkoa wa Manyara, Ally Msuya alisema wamekua
na mahusiano mazuri na NMB hiyo kupitia umoja wao ambao wameutumia kutatua
changamoto za wafanyabiashara wanaochipukia na wenye uzoefu wa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment