Naibu Waziri wa Afya Maendeleo Ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto Dk. Faustine Ndugulile (pichani), amesema, Serikali ina mpango wa
kuanza kutoa oparesheni za ubongo nchini kwa kutumia matundu ya ubongo
ili kupunguza athari za kiharusi.
Ndugulile
amesema hayo jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea
mabanda yaliyo chini ya Wizara hiyo, katika maonesho ya 43 ya biashara
ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika barabara ya
Kilwa.
Amesema serikali
inaiagiza Muhimbili kufanya tafiti kwa magonjwa yanayosambazwa na
mbu kwani amekuwa akibadilika sana kitabia.
"Kuna
mbu anaitwa Aedes anayeeneza ugonjwa wa Dengue, mwingine Anofeles
akisambaza malaria n'a yule wa matende n'a mabusha...waliokuwa wakiuma
mchana wamebadilika n'a kuuma usiku n'a vivyo vivyo kwa wale
waliokuwa wakiuma usiku, " Amesema Ndugulile.
Amesema
mabadiliko hayo ya mbu inatakiwa utafiti, kwani mbu waliokuwa
wakikaa ndani sasa wapo nje, n'a wale waliofikiriwa kuuma ndani tuu
kumbe sasa wanauma nje.
"Nafikiri
kuna mbu wa ndani tuliokuwa tukiwakinga kwa chandarua lakini
ikabainika kwa sasa wanauma nje hivyo jitihada za kuhamasisha
matumizi y'a chandarua ikawa hayana tija, mbu wengine waliokuwa
wakiruka juujuu sasa wanaruka chinichini, "amesema.
Amesema
watafiti hao wafanye utafiti kuangalia tabia hizo pamoja na dawa
zinazoweza kuua mbu pamoja na viuadudu kama vinafanya kazi nzuri.
"Katika
banda la Muhimbili wanaonyesha dawa za kufukuza mbu n'a hata
mafuta ya kukupata kwa ajili ya kufukuza mbu," amesema.
Amesema Hata Taasisi y'a Utafiti wa Magonjwa yanayosambazwa Binadamu (NIMR) tumeshawambia katika kutekeleza suala hilo.
Kuhusu
operesheni za ubongo alisema Taaisi y'a Mifupa y'a MOI inafanya
operesheni hizo n'a wapo wataalam waliokwenda Nchini China
wakitarajiwa kurudi hivi karibuni.
Amesema operesheni hizo itakuwa za tundu Ndogo, wakiziba damu katika mishipa n'a kupunguza athari za kiharusi.
No comments:
Post a Comment