Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kukagua maandalizi ya
mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC katika jengo la pili na la tatu
kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es
salaam, Julai 31, 2019. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia
Mjema. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es
salaam wakati alipokagua maandalizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano
wa SADC kwenye Jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Wilson Kantambula (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Damas Ndumbaro (kushoto)
wakati alipokagua maadalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC
kwenye jengo la pili na la tatu katika kiwanja cha ndege cha Julius
Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya mapokezi ya wajumbe
wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu la abaria katika
kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo
la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona
maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.
Akizungumza na watendaji wa Serikali
pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31,
2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.
“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri,
lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka,
vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,”
amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi
hilo.
Katika jengo la tatu la abiria kwenye
uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia,
watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua
vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.
Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado
hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya
kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe,
vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over,
bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.
Amewataka
wahusika waweke banners za kutosha za
aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna
mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.
Wakati
huohuo,
Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa
kuendesha biashara zao na ujasiriamali.
“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano
huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea
uchumi,” amesema.
No comments:
Post a Comment