Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali, Vicky Bishubo, akikabidhi vifaa
mbalimbali vikiwemo kompyuta, madaftari na madirisha ya aluminium kwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
kwenye shughuli iliyofanyika zahanati ya Nandangala wilayani Rukwa.
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi, kompyuta, na Madaftari
vyenye thamani ya Tsh. Milioni 25 kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu na
afya katika halmashauri ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Vifaa
hivyo vimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae pia ni
Mbunge wa jimbo hilo katika Zahanati ya Nandagala iliyopo katika Kijiji
cha Nandagala Wilayani humo.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali Bi, Vicky Bishubo alisema
Vifaa hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Madilisha ya Aluminium kwa ajili
ya Zahanati ya Nandagala yenye thamani ya Tsh. milioni 15, mabati 56
zikiwa na Mbao zake za kupaulia vyenye thamani ya Tsh. Milioni 3.3,
Kompyuta 10 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kasimu Majaliwa pamoja na
Madaftali yenye thamani ya Tsh. Milioni 5 kwa ajili ya Shule mbali mbali
katika Wilaya hiyo ya Ruangwa.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Idara ya Huduma za
Serikali Bi, Vicky Bishubo kwa niaba Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Benki
hiyo Albert Jonkergouw alisema kuwa kwa NMB changamoto za sekta ya Afya
na Elimu hapa Tanzania ni jambo la kipaumbele kutokana na umuhimu wa
sekta hizo kuwa ndio nguzo kuu ya maendeleo kwa Taifa.
“Sisi
kama NMB tumekuwa msitari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa
lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii, ambapo kwa zaidi ya
miaka saba mfululizo tumeweza kuchangia 1% ya faida yetu kama sehemu ya
uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka” alisema Bishubo
Hata
hivyo Bishubo aliongeza kuwa kwa mwaka 2019 Benki yao imetenga kiasi
cha Tsh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo
kusaidia sekta ya Elimu na Afya ambapo mpaka sasa tayari imeshatoa
msaada wa zaidi ya Tsh. Milioni 600.
Akizungumza
baada ya kupokea vifaa hivyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliishukuru
Benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ikiwa ni moja ya kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano
Majaliwa
alisema kama Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki
hivyo katika shughuli mbali mbali za maendeleo pamoja na majanga
yanapotokea.
No comments:
Post a Comment