NA
TIGANYA VINCENT
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) inatarajia kuwafikisha mahakamani
Askari 6 wa Jeshi la Polisi na watendaji watatu wa vijiji wilaya Igunga baada
ya kuomba rushwa shilingi milioni 8.
Akizungumza
na vyombo mballimbali vya habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani
Tabora Musa Chaulo alisema kwamba watu hao watafikishwa Mahakamani baada ya
uchunguzi kumamilika.
Alisema
kwamba watendaji hao wa serikali wasio waaminifu walimuomba rushwa mzee Ngaka
Mataluma Fale (95) baada ya kumukamata wakimtuhumu kuwa anajihusisha na tiba
asilia bila kibali, kukutwa na mfupa unaodaiwa kuwa binadamu, kumiliki silaha
za moto , kukutwa na mafuta ya simba, ngozi ya kengee na kukutwa na bangi.
Chaulo
alisema baada ya Fale kukosa kiasi hicho cha fedha alitakiwa kuuza ng’ombe ili
apate kiasi hicho cha milioni 8 kwa ajili ya kutoa hongo kwa Maafisa
waliomkamata.
Aliongeza
kuwa TAKUKURU ilifanikiwa kuwakamata ng’ombe kumi na mmoja wa Fale katika Mnada
wa Igunga kwa wanunuzi wakijiandaa kuwasafirisha kwenda Arusha na kuongeza kuwa
baada ya kuwakamata imewarajesha kwa mhusika.
Katika
hatua nyingine Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Tabora Chaulo amesema katika
robo iliyoishia Juni , 2019 imefuatilia na kukagua miradi arobaini ya maendeleo
yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 9.285.
Alisema
kati ya miradi hiyo saba inayohusu sekta ya elimu, afya na ujenzi zenye thamani
ya shilingi bilioni 1.570 inafanyiwa
uchunguzi mwisho
No comments:
Post a Comment