NA TIGANYA VINCENT
WADAU wa maendeleo Mkoa wa Tabora wametakiwa kuandaa mpango mkakati
utakaougeuza mkoa huo kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji ili kuchangia na kuinua uchumi wa Taifa kwa
kuwaunganisha wajasiriamali na wawekezaji wakubwa
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri wakati wa mkutano wa kujadili na kutengeneza mkakati wa kuboresha mazingira ya
uwekezaji mkoani humo
Alisema mipango hiyo ni lazima
ilenge kuongeza uzalishaji wa malighafi mbalimbali zikiwemo za kilimo ambazo
zitasaidia ujenzi wa viwanda ili kuongeza thamani na tija kwa wakulima.
Mwanri alisema kwamba uchumi
wa kati wa viwanda, utakuza maendeleo endelevu na kuuwezasha Mkoa kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora ambazo
zinaweza kuuzwa nje ya nchi.
Alisema ili Taifa liweze kuufikia uchumi wa kati, ni lazima sekta
binafsi ziimarishwe ili ziwe na uwezo wa uzalishaji mali kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo ambavyo
ndiyo msingi wa ukuaji wa viwanda vikubwa na unaozalisha bidhaa zinazotumiwa nchini.
Naye
Meneja wa Kituo
cha Uwekezaji Kanda ya Magharibi (TIC) Innocent Kahwa alisema asilimia kubwa ya
pato la watu binafsi linategemea wawekezaji na wafanyabiashara wadogo na wakati .
Alisema
ili kupata mafanikio katika uwekezaji ni vema kujenga mazingira ya kuaminiana
kati ya sekta binafsi na Serikali ili kila pande ifanye kazi zake kwa uhuru na
kuwawezesha wajasiriamali kupata ubia.
No comments:
Post a Comment