HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 22, 2019

SERIKALI KUJENGA CHUO CHA VETA MINYUGHE WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA

 Mbunge  wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika   Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida.  
 Mbunge  wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akilakiwa na wakina mama alipo kuwa amewasili kwenye mkutano huo.
 Mbunge  wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiwasalimia wananchi alipokuwa amewasili kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi, Jafari Dude akizungumza kwenye mkutano huo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Minyughe, Nelson Kiwesi,  akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Minyughe, Samuel Daniel,  akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amesema Serikali imetenga zaidi ya sh.bilioni
mbili kwa ajili ya kujenga Chuo cha Ufundi Veta cha kisasa katika Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kingu aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia Wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuzungumzia miradi ya maendeleo iliyofanyika kwenye kata hiyo na kujua changamoto zilizopo.

"Tuna bahati sana sisi Wanaminyughe kwani serikali yetu sikivu inayoongonzwa na Rais Dkt.John Magufuli inatuletea chuo cha Veta katika kata hii tunakila sababu ya kuichagua kwa kura nyingi mwakani" alisema Kingu.

Alisema ujenzi wa chuo hicho ukikamilika kitasaidia watoto wa wilaya hiyo na maeneo mengine wanao maliza elimu ya msingi na sekobdari kwenda kupata stadi mbalimbali za ufundi na kuweza kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa nchini.

Diwani wa Kata ya Minyughe Samuel Daniel alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na nchi nzima kwa ujumla.


Daniel alisema tayari wamekwisha tenga eneo la ekari 54 kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho ambacho kitakuwa mkombozi kwa watoto wa kata hiyo na mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

Pages