HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2019

WANANCHI WATAKIWA KUFIKA BANDA LA TAEC KATIKA MAONESHO YA SABASABA KUPATA TAARIFA KUHUSU MIONZI


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo (kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika bando lao lililopo kwenyeMaonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo (kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika bando lao lililopo kwenyeMaonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo (kulia), akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika bando lao lililopo kwenyeMaonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam leo.

Wananchi wakipata taarifa kuhusu mionzi.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo, akigawa vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali kuhusu tume hiyo.


Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomiki, Peter Ngamilo (kushoto), akimkaribisha Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, alipotembelea banda la tume hiyo kwenye Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, akisaini kitabu cha wageni alipofanya ziara katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania kwenye Maonyesho ya 43 yua Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akifafanua jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Peter Ngamilo wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya JK Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sylvia Lupembe.




Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam


TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara maarufu kama sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam, ili kupata elimu ya matumizi mbalimbali ya mionzi na kuweza kutambua maeneo ambayo yana mionzi.


Mtafiti wa Masuala ya Nyuklia, Alex Muhulo, ambaye alikuwa kwenye banda lao, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mbali na hilo, pia wanatoa elimu ya kuangalia na kutambua vituo ambavyo vimepimwa, vimedhibitiwa na vimepewa leseni ili kujua kama kituo cha afya kimekaguliwa.

"Dhima ya tume hii ni kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma, wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu.

"Hivyo tunawakaribisha wananchi kutembelea banda letu ili kupata elimu hii, na kuweza kufahamu vitu mbalimbali," amesema.

Akizungumzia madhara ya simu ya mkononi, Muhulo amesema simu inamadhara ya mionzi isiyo ayonishi, ambapo madhara yake hayaonekani moja kwa moja.

"Mfano ukitumia simu muda mrefu inaleta joto ambalo linaweza kuleta madhara kwenye ubongo au sikio. Hivyo tunawashauri ili kuepuka madhara hayo kutumia loudspeaker au headphone ambavyo vitaweza kukufanya kuongea muda mrefu na kuepuka hayo madhara," amesema.

Hata hivyo amesema tume kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wana kikosi kazi ambacho kinasaidia kupima simu na kuhakikisha simu zinazoingia nchini zinakuwa na viwango.

Pia Muhulo ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanawafikia wananchi wa urahisi, tayari mpaka sasa ina ofisi 21 katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages