Brasilia, Brazil
Ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanyabiashara kutoka sekta binafsi na baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma wamefanya ziara ya kibiashara nchini Brazil yenye lengo la kutafuta fursa za kibiashara, uwekezaji na masoko kwa bidhaa zinozalishwa Tanzania.Ziara hii ilianza tarehe 28 Juni hadi 08 Julai,2019.Ziara hiyo ya siku kumi imebuniwa na sekta binafsi kwa mashirikiano na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia, imejumuisha washiriki kumi na mbili ( 12) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, ofisi ya ubalozi wa heshima wa Brazil nchini Tanzania, jumuiya ya wafanya biashara Tanzania; kampuni ya Zest limited na Kampuni ya Alpha Group Afrika.
Washiriki wengine katika ziara hiyo ni kampuni
ya KC Land Development Plan, Kampuni ya Pivotec Company Ltd pamoja na
Shirika la biashara la Taifa la Zanzibar(ZSTC), Mamlaka ya Uthibiti wa Matumizi
wa Maji na Nishati Zanzibar(ZURA) na LAM Consultant.
Katika Ziara hiyo ujumbe wa Tanzania umeonana na kufanya mazungumzo na Taasisi mbali mbali za Brazil zikiwemo shirika kuu la uchimbaji mafuta na gesi la Brazil (Petrobras), kampuni ya shughuli za idhibiti wa viwango na uendelezaji wa masoko ya mafuta na gesi (IBP), Wakala wa uwekezaji na Biashara ya Brazil (APEX), Muungano wa Jumuiya ya Wenye viwanda ya Brazil (NCI) na Taasisi ya Uendelezaji wa Wazalishaji wadogo na Wakati (SEBRAE).

Taasisi nyingine ambazo ujumbe huu ulikutana
na viongozi na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano ni Bodi ya Utalii ya
Brazil(Embratur), Wizara ya Kilimo, Sehemu ya udhibiti wa biashara za Mazao ya
matunda na mifungo, Muungano wa Wenye viwanda wa São Paulo na Taasisi ya
uendelezaji wa Teknolojia na ubunifu (São Paulo Technlogy Incubator) ya mjini
São Paulo.
Hali kadhalika, ujumbe wa Tanzania ulipata
nafasi ya kutembelea Miji mbali mbali ya Brazil ikiwemo Rio de Janeiro ,
Brasilia, na São Paulo pamoja na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi na
Maofisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Brasilia na
kukutana na Jumuiya ya Watanzania (Diaspora)
waishio mjini São Paulo.
Katika mazungumzo na shirika la uchimbaji wa mafuta na gesi la Petrobras na Kampuni ya uendelezaji wa masoko na Udhibiti wa mafuta na gesi (IBP) ilibainika kwamba pamoja na kampuni ya Petobras kusitisha shughuli zake za utafutaji wa mafuta nchini Tanzania, nchi hizi mbili zinaweza kuendeleza kushirikiana katika maeneo mbalimbali yakiwepo kujenga Uwezo, kuendeleza utafiti, kukuza masoko na shughuli za udhibiti wa bidhaa na viwango katika sekta ya mafuta na gesi, pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu. Ili kuhakikisha utekelezaji wa maazimio yaliyokubaliwa pande mbili (IBP na Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania-ATOGS) zimekubaliana kuandaa mkataba wa ushirikiano na kusainiwa mara baada ya kukamilisha taratibu zinazohitajika.
Kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa bidhaa za Tanzania kama vile korosho, karafuu na mazao ya bahari kupata soko nchini Brazil. Pia wajumbe wamebaini kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Tanzania kununua sukari kutoka Brazil. Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia umeahidi kufuatilia upatikanaji wa masoko hayo. Brazil ni mzalishaji mkubwa wa sukari na mazao ya mifugo.

Katika mazungumzo yaliyohusu
ushirikiano wa uwekezaji kati ya nchi mbili yaliyofanyika katika Makao
makuu ya wakala wa uwekezaji wa Brazil (APEX) mjini BrasÃlia ilibainika kuwa
Tanzania ina nafasi kubwa ya kujifunza katika taratibu za kuvutia wawekezaji
kutoka nje na kuendeleza wawekezaji wa ndani.
Pia pande mbili zilikubaliana
kushirikiana katika kuendeleza fursa za uwekezaji na kubadilishana Taarifa.
Vile vile wajumbe walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuwa na taarifa za kutosha
kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, hivyo wito ulitolewa kwa ofisi za
Ubalozi wa Tanzania Brasilia, Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania, wakala wa
uwekezaji wa Brazil , mamlaka za uwekezaji Tanzania na jumuiya ya wafanya
biashara na sekta binafsi Tanzania kuimarisha ushirikiano wa karibu sana kwa
lengo la kuimarisha uwekezaji na kukuza biashara kwa maslahi ya maendeleo ya
uchumi wa nchini hizi mbili.
Kutokana na ziara hii, ujumbe wa
Tanzania pia ulipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa Taasisi inayohusika na
kuendeleza wazalishaji wadogo wadogo na wa kati (SEBRAE) nchini Brazil.
Mazungumzo hayo yalifanyika katika makao makuu ya ofisi hiyo yaliyopo mjini
Brasilia.
Baada ya mazungumzo hayo pande mbili zimekubaliana kuimarisha
ushirikiano katika maeneo ya kubadilishana wataalam, uzoefu, na kujenga uwezo
hasa kutokana na nchi ya Brasil kupiga hatua kubwa na kufanikiwa kuleta maendeleo
katika kuimarisha uwezo wa wazalishaji wadogo wadogo na wa kati hasa wanawake.
Pia ujumbe wa Tanzania ulitoa mwaliko kwa Viongozi wa taasisi hiyo na baadhi ya
wazalishaji wa Brazil kutembelea Tanzania mwezi wa Oktoba wakati wa Tanzania
Expo.
Kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa Tanzania na Jumuiya ya Muungano
wa viwanda wa Brazil, pande mbili zimekubaliana kwamba nchi hizi mbili
zinashabihiana kimazingira, kijiografia, mila na utamaduni. Hivyo kuna haja
kubwa wa kuimarisha mahusiano, kubadilishana wataalam, habari, na kukuza
technologia ya uzalishaji katika viwanda.
Brazil imeonesha nia ya kusaidia
Tanzania katika kujenga uwezo wa wataaman wake kwa kutumia taasisi zake za
mafunzo ya Technologia na kuendelea uzalishaji katika sekta ya viwanda.
Kwahivyo imeonekana kwamba kuna haja ya kuweka saini makubaliano ya ushirikiano
wan chi hivi mbili kati ya Jumuiya ya Muungano wa Viwanda wa Brazil na Jumuiya
ya sekta binafsi pamoja na Jumuiya ya wafanyabiashara, wenye viwanda na
wakulima wa Tanzania. Hatua hiyo itafikiwa baada ya kukamilisha taratibu za
mikataba ya kimataifa
Kwa upande wa utalii imebainika kwamba licha ya kuwa Brazil na Tanzania kuwa zina mazingira na vivutio vinavyolingana vya utalii, Brazil inapokea zaidi ya mara tatu ya idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania. Hivyo Tanzania ina mengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Brazil. Wito umetolewa kwa pande mbili kushirikiana kwa kubadilishana uzoefu, taarifa na utaalamu pamoja na kutembeleana.
No comments:
Post a Comment