Abdul Athuman kutoka Chuo Cha Watu Wenye Ulemavu (VTC) Singida, akionyesha kipaji alichonacho cha ushaonaji.
Mwanafunzi wa Chuo Watu wenye Ulemavu Sabasaba VTC Singida kilichochini ya Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Zanura Mohamed akiwaonesha watu waliofika katika Viwanja vya maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara katika banda la VETA jinsi ya kushona nguo.
Na Janeth Jovin
CHUO cha watu wenye ulemavu Sabasaba VTC Singida kilichochini ya Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kimewataka walemavu kujitokeza kusoma mafunzo ya ufundi ili waweze kujiajili ama kuajiliwa.
Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa na Biashara, Mwalimu fani ya ushonaji katika chuo hicho, Frola Patrick anasema anaomba walemavu kujitokeza kupata elimu ya ufundi stadi ili waweze kujiajili.
Anasema walemavu wengi wanashindwa kujitokeza kusoma wakidhani kwamba hawawezi kufanya shughuli zozote za uzalishaji maji jambo ambalo amesema si kweli.
"Katika chuo chetu tunawafundisha walemavu kutengeneza batiki, pochi kwa kutumia vibao, ushonaji wa mavazi ya kike na kiume pamoja na uselemara hivyo tunawaomba walemavu wajitokeza kwa wingi katika chuo hichi ili waweze kupata elimu, " anasema.
Hata hivyo anasema moja ya changamoto wanayokumbana nayo katika chuo hicho ni wazazi kuwaleta wanafunzi ambao awajui kusoma wala kuandika.
Naye mwanafunzi katika chuo hicho, Zanura Mohamed anasema mafunzo ya ufundi stadi aliyoyapata katika chuo hicho yamemsaidia kutokuwa tegemezi kwa wazazi wake.
"Mimi sasa hivi nafuma na kushona nguo, vitu ninavyovifanya nikuviuza napata kipato cha kujikimu na maisha yangu jambo ambalo linaniondolea kuwa tegemezi, " anasema.

No comments:
Post a Comment