HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2019

WABUNIFU WAFUATWE VIJIJINI: SERIKALI

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akitembea katika viwanja vya Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).

Mgunduzi wa Mfumo wa Jua kwa ajili ya kufundishia shuleni, Ernest Maranya, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha.



Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam

SERIKALI imeagiza wabunifu mbalimbali nchini kufuatwa maeneo ya vijijini ili waweze kuonesha kazi zao kutumika na kuleta manufaa kwa taifa.

Hayo yalielezwa leo Julai 3, 2019 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alitembea katika viwanja vya maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda hayo, amesema amefurahishwa na kazi zao lakini wasiishie katika maelezo tu waandae kwa vitendo zaidi.

"Nimeona jinsi mlivyojiandaa vizuri kiukweli nawapongeza, lakini nimeona wengi wenu mmeandaa makaratasi tu kuwaeleza watu, haya ni maonesho hivyo waonesheni watu bidhaa zenu," amesema.

Ameongeza, "Mfano nikiwa katika banda la Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA ) nimeona wabunifu wa mitambo ya umeme unaosaidia katika masuala mbalimbali ya kiusalama hii itasaidia mkaweza hata kuwapa mitaji wakafanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na mashirika makubwa kama vile ya Umeme nchini (TANESCO),"

Katika banda la VETA kuna mbunifu amefanikiwa kutengeneza mfumo unaopiga simu kama eneo la nyumba  lina hatari.

"Nimetembelea mabanda takribani nane yaliyokuwa chini ya Wizara hii lakini nimeona kuna wabunifu wengi wapo na wanabuni kazi mbalimbali zenye uwezo mkubwa wa kusaidia taifa hili hivyo ni vyema wakafuatwa katika maeneo yao na COSTECH mkawa katika mstari wa mbele kuwasaidia wabunifu hao," amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages