Mkuu
wa chuo cha Uhasibu Prof.Eliamani Sedoyeka pamoja na wa wilaya ya
Longido Frank Mwaisumbe wakisikiliza maelekezo ya mwanafunzi wa chuo
cha uhasibu Arusha wakati walipotembelea Maonyesho ya chuo cha Uhasibu
kwa wanafunzi wa shule za sekondari 18 za wilaya ya Arusha yanayofanyika
chuo hapo jijini Arusha.
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Wito
umetolewa kwa wanafunzi wa sekondari nchini kuona umuhimu wa kujiandaa
wao kwa masomo ya mitaala ya vyuo vikuu watakavyochukuwa wakati wa
kujiunga kwa kuwa na uelewa wa masomo watakayoyachagua na kuyachukuwa.
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe kwa niaba ya
mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya chuo
cha Uhasibu kwa wanafunzi wa shule za sekondari 18 za wilaya ya Arusha
iliyofanyika chuo hapo jijini Arusha.
Mwaisumbe
amesema kujiandaa mapema kunasaidia wanafunzi hao kuzoea mazingira ya
masomo ya elimu ya juu kwani wakifanikiwa wanapata uzoefu wa kuzoea fani
mbali mbali zinatotolewa na vyuo hivyo.
Amehimiza
chuo cha uhasibu kuendeleza maonyesho hayo kwa lengo la kuwaandaa
vijana kuweza kufikia ndoto zao za kitaaluma na wasiishie kwenye wilaya
ya Arusha pekee na waende mbali zaidi katika mkoa mzima na nchi kwa
ujumla.
Awali
Mkuu wa chuo cha Uhasibu Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kuwa maonyesho
hayo yanalengo kubwa la kuwapa nafasi vijana waliopo sekondari kidato
cha nne na sita kwa ajili ya kujiandaa kuchukuwa kozi anayopenda
itakayomsaida kufikia ndoto zake.
Amesema
kwamba maonyesho hayo yatawasaidia wanafunzi hao kukutana na wataalamu
na wakufunzi wa chuo hicho pamoja na wanafunzi kujionea taaluma
mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho na kubadilisha mawazo ya kufikia
elimu ya juu.
Amesema
kuwa mwisho wa maonyesho hayo wanatarajia kupata wanafunzi wengi
watakaopenda kujinga na mafunzo chuo hapo kama lilivyo lengo la chuo
hicho na uwepo wake unategemea wanafunzi kuweza kujiendesha.
Maonyesho
hayo pia yamelenga namna ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa lengo
la kuwasaidia vijana kuweza kujiajiri na kutotegemea kuajiriwa jambo
litakalosaidia azma ya serikali ya uchumi wa kati wa viwanda.
No comments:
Post a Comment