Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea
hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakatia akifungua mafunzo
hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama,
Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Na
OWM, ARUSHA
Wataalam
wa maabara nchini kwa kutumia Dhana ya
Afya moja ambao ni wataalam wa maabara
kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja
na
mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya Usimamizi na udhibiti
wa vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama
wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi vya kibailojia vinaweza sambaza magonjwa kwa
wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa
kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa
kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi
pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya
kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo
tarehe 29, Julai, 2019, Mratibu wa Afya
Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo
ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya
Usimamizi na Usalama wa vimelea
hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.
“Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu
kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana za vihatarishi vya kibaiolojia,
ikiwemo wakati wa kusafirisha
vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia
wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya
kuvifanyia uchunguzi” amesema Chinyuka
Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa
mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada
ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa maabara itazingatia usalama wa afya zao na
usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia
na kudhibiti vihatarishi vya kiulinzi na
usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa
dhamana ya kuvifanyia kazi.
Mafunzo
hayo ya siku tano, yameandaliwa na DTRA na Sandia National Laboratories na
wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia ,
Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo, chini ya Uratibu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu.
Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu ,
wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na
kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.
No comments:
Post a Comment