HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 22, 2019

BENKI YA DUNIA YAPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUTOA KIPAUMBELE KWENYE SEKTA ELIMU

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati), akimpokea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari ya Kibasila. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Yasinta Matilya. Shule hiyo kongwe imepata Sh. Milioni 900 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo iliyojengwa mwaka 1951. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Yasinta Matilya, akizungumza katika mkutano wa ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watumishi wa shule hiyo uliofanyika shuleni hapo Agosti 22, 2019.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Yasinta Matilya, akimkabidhi hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Gerald Mweli, akizungumza katika mkutano huo.
Mwalimu akiuliza swali.
 Mwalimu Masebu akiuliza swali.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kutembelea Shule ya Sekondari ya Kibasila jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Kibasili, alipofanya ziara shuleni hapo ambapo shule hiyo imenufaika na fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo.
 Baadhi ya walimu waliohudhulia mkutano huo.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (wa nne kulia), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Yasinta Matilya, akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo (hawapo pichani), wakati ujumbe wa Benki ya Dunia ulipofanya ziara shuleni hapo.
 Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza mgeni rasmi.
 Mwanafunzi akiuliza swali.
 Meza Kuu.
 Wanafunzi.
 Meza Kuu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila (hawapo pichani).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Kibasila.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kibasila Sekondari.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kibasila Sekondari.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, wakiwapungia mikono wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila.
 Kubadilisha mawazo.
 Kuagana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe, akiaga na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako. 
 Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Yasinta Matilya, akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Anne Kabagambe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akiagana na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila, Yasinta Matilya.

 

Dar es Salaam, Tanzania

Benki ya Dunia imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele  kwa sekta ya Elimu na kwamba ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa sana katika kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata nafasi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa jijni dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia ukanda wa nchi za Africa Anne Kabagambe alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Kibasila akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.

 Mkurugenzi huyo

 ametembelea shule ya Kibasila kwa sababu Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi zinazofanywa katika sekta ya elimu ikitambua kuwa elimu ndio chimbuko la maendeleo katika nchi yoyote

Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema Benki ya Dunia imekuwa ikishirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo  ikiwemo mradi wa Elimu unaojulika kama Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo Benki ya Dunia imetoa dola za kimarekani milioni 202 katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2014 na unategemewa kumalizika mwaka 2021.

Waziri Ndalichako amesema kupitia mradi huo takribani Sh bilioni 141 zimeshatumika kwa ajili ya kukarabati shule kongwe 62, kujenga vyumba vya madarasa 2,876, matundu ya vyoo 6,558, nyumba za walimu 59, mabwalo 76, majengo ya utawala 16, Mabweni 533 kwa ajili ya kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za mbalimbali, pamoja na kujenga mifumo ya maji safi kwenye baadhi ya shule ambazo hazikuwa na vyanzo vya maji.

Aidha Waziri Ndalichako alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari Kibasila  Sh. shilingi milioni 900 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020  kwa ajili ya ukarabati na tayari wataalamu  wameanza kufanya tathmini ya majengo ya shule hiyo ambayo ukarabati wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa.

Awali akitoa taarifa ya  shule Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Yasinta Matilya amesema moja ya changamoto inayokabili shule hiyo ni utoro wa wanafunzi unaotokana na changamoto za kifamilia ikiwemo watoto kulelewa na mzazi mmoja, kipato duni, umbali wa makazi ya wanafunzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hiyo wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa saikolojia watakaowasaidia kujitambua ikiwa ni pamoja na kuwajengea mabweni ili kuepukana na vishawishi vya barabarani pamoja na usumbufu wa usafiri wa unaopelekea wanafunzi kuacha shule. 

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 

22/08/2019

No comments:

Post a Comment

Pages