MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) umeandaa Tamasha la Jinsia ambalo litafanyika kuanzia Septemba 24 hadi 27, mwaka huu.
Tamasha
hilo ambalo litakuwa la 14, litafanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao
vilivyopo Mabibo jijini Dar es Salaam, huku wanawake zaidi ya 1000
wakitegemewa kuhudhuria.
Akizungumzia
tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi
alisema tamasha hilo litakwenda sambamba na kuangalia miaka 25 ya
harakati za ukombozi wa wanawake nchini.
Alisema katika tamasha hilo, kutakuwa na mijadala mbalimbali pamoja na kuangalia miaka 25 tangu lilipotolewa azimio la Beijing.
"Pia
tutasherehekea miaka 25 ya TGNP pamoja na kuadhimisha miaka 25 ya
mpango kazi wa Beijing kutafakari ni wapi tulipotoka na tulipo, na nini
kifanyike ili tuweze kusonga mbele," alisema Liundi.
Kwa upande wake Ofisa Mwandamizi wa Programu ya ujenzi wa nguvu za pamoja kutoka TGNP, Anna Sangai alisema
bado
jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu mila na desturi potofu kwani
masuala ya jinsia hayawezi kufikiwa kama bado chagamoto hizo zipo.
"Hatuwezi
kufikia masuala ya kijinsia kama bado hivi vitu vinaendekezwa. Kuna
uhitaji mkubwa wa watu kufahamu masuala ya jinsia," alisema Sangai.
No comments:
Post a Comment