Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama, akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji ya Benki ya I&M jijini Dar es Salaam Agosti 26. (Picha na Francis Dande).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

Mkuu wa Idara ya Wateja wa RejaReja Benki ya I&M, Lilian Mtali.
Meza Kuu.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Baseer Mohammed, akizungumza katika uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji.
Baadhi ya wageni waalikwa.
Meneja Msaidizi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji Benki ya I&M, Frank Bunuma, akizungumza kuhusu Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji iliyozinduliwa na benki hiyo.
Na Janeth Jovin
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezitaka Benki za biashara nchini kuanzisha huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji katika masoko ya mitaji kwa lengo kuongeza idadi ya wawekezaji.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama wakati akizindua huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji katika Benki ya I&M.
Mkama alisema hatua ya uanzishwaji wa jambo hilo itazisaidia benki hizo kuongeza idadi ya wawekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Alisema huduma hiyo ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji utawezesha na kurahisisha biashara kwa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa.
Aidha Mkama ametoa wito kwa benki hizo kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ikiwemo kuuza dhamana kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam ili kuongeza mitaji yao.
"Hatua hii itasaidia utekelezaji wa agizo la Serikali kwa benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha ili kuweza kujiendesha kibiashara, " alisema.
Hata hivyo Mkama amezitaka kampuni za bima pia kutumia fursa zilizopo Katuma sekta ya masoko ya mitaji ili kuongeza mitaji yao na kuongeza kuwa jambo hilo litaziwezesha kampuni hizo kuwa na uwezo wa kushindana na zile za nje zinazotoa huduma ya bima hapa nchini.
"Vilevile natoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na taasisi za fedha kuunga mkono malengo na azma ya serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda kupitia masoko ya mitaji nchini, " alisema Mkama.
Naye Meneja Msaidizi wa Benki ya I&M kitendo cha Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji, Frank Bunuma alisema benki hiyo inaendelea kukua kwa kasi kutokana na kutoka kuwa taasisi ya fedha ya jumuiya hadi kuwa benki ya biashara.
Alisema benki hiyo imeamua kuanzisha huduma hiyo ya usimamizi wa dhamana na uwekezaji kwa lengo la kuwasaidia wawekezaji katika kuwapa elimu juu ya namna na mahali pazuri pa kuwekeza.
"Uanzishwaji wa huduma hii ni ushahidi tosha wa benki kuendelea kusimamia dhamira yake Ya kuwa benki imara zaidi, tunatambua kuwa hii ni fursa nzuri kwa wawekezaji wa Tanzania kuwekeza katika masoko ya mitaji na dhamana ndani ya nchi pamoja na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, " alisema Bunuma.

No comments:
Post a Comment