MANCHESTER, ENGLAND
KLABU ya Manchester City imeongeza muda wa ushirikiano rasmi
wa mauzo ya moja kwa moja na kampuni ya QNET yenye maskani yake barani Asia.
Kurefushwa kwa ushirikiano baina ya pande hizo mbili,
kumekuja baada ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa kipindi cha miaka 10, wakiwa
wauzaji wa moja kwa moja wa timu ya wanawake na wanaume ya Man City.
Aidha, ushirikiano huu unaashiria mafanikio zaidi tangu Mei,
Mwaka 2018 pale Klabu hiyo ilipoikaribisha QNET kama mshirika wa kwanza wa lebo
za mikononi katika Ligi ya Wanawake ya Super League.
Chini ya makubaliano hayo, kipindi chote cha ushirikiano huu
kampuni ya QNET itaendelea kutoa kliniki za soka zinazosimamiwa na klabu hiyo kwa
jamii kote duniani na kujihusisha na watumiaji na wasambazaji.
Katika kusherehekea tangazo hilo, QNET imezindua toleo dogo
la saa za mkononi inayojulikana kama 'QNETCity Champions' zinazoundwa na kuzalishwa
na mafundi mahiri wa nchini.
Makamu wa Raisi Mwandamizi wa ushirikiano wa Man City Football
Group, Damian Willoughby, alitoa maoni yake na kusema;
"Tuna furaha
kutangaza kuwa QNET imekuwa mshirika wa hivi karibuni.
“Tumeongeza muda wa ushirikiano na Man City katika
makubaliano ya muda mrefu ambayo yatashuhudia tukisherehekea miaka kumi ya
kufanya kazi kwa pamoja.
“Ushirikiano huu uliweka historia pale QNET ilipokuwa mshirika wa kwanza wa lebo za mikononi, katika
ligi ya wanawake ya Super League na tuna furaha kuingia katika ukurasa mwingine
kwa pamoja."
“Mkurugenzi Mkuu wa QNET, Malou Caluza alisema: “Huu ni
ushirikiano unaothaminiwa sana kwa QNET
na Man City kwa sababu utendaji bora ni msingi wa chapa zote mbili.
“Sote tuna msukumo kuelekea katika mafanikio kwa kufanya kazi
kwa bidii, ari na kujitolea.
“Kupitia ushirikiano huu, tumeweza kuwa na fursa ya
kuwapeleka watoto kutoka katika familia zenye kipato kidogo kutoka maeneo
mbalimbali duniani kwenda Man Utd kwa ajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa
miguu na kozi ya lugha ya kiingereza.
“Kweli, imekuwa ni fursa
nzuri sana ya kubadilisha maisha kwa watoto walio wengi. Tunatumaini kuwa
tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja na kutafuta njia mpya za kibunifu za
kushirikiana na kuwafikia mashabiki wetu." Alisema.
QNET ni moja kati ya makampuni ya mauzo ya moja kwa moja kutoka
Asia yanayoongoza ambayo inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo
ya maisha ambayo yanasaidia watukuishi maisha bora zaidi.
Kwamiaka 20, Mtindo wa biashara ya kuanzia ngazi ya chini ya
QNET umeongezewa kasi na nguvu ya biashara ya mtandao imesaidia kuwawezesha mamilioni
ya wajasiriamali katika nchi zaidi ya 100 duniani kote.
No comments:
Post a Comment