Mwezeshaji Andochius Kamuhabwa akiwa na Mratibu wa Shirika la FARAJA FOR HOPE AND DEVELOPMENT
ORGANISATION, Shakira Omary.
Na Lydia Lugakila, Kagera
Wananchi katika Halmashauri ya Wilaya
ya Bukoba mkoani Kagera wamehimizwa kufuatilia miradi mbali mbali ya maji
inayoletwa katika maeneo ya ili kujua
Bajeti ya miradi hiyo na ukidhi wa viwango jambo litakalosaidia
kutopokea miradi hewa.
Kauli hiyo imetolewa na Shakira
Omary ambaye ni mratibu wa Shirika la FARAJA FOR HOPE AND DEVELOPMENT
ORGANISATION shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na uwajibikaji,
ufuatiliaji wa jamii katika sekta ya maji lilopo katika kata ya Nshambya
manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Omary amesema kuwa wananchi ni
Chachu ya maendeleo ya taifa hivyo wananchi wanapaswa kufuatilia kila miradi iliyopo
katika maeneo yao kwa sababu mwananchi anachangia kwa asilimia mia moja katika miradi hiyo.
Amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa woga katika kuhoji viongozi
wanawaletea miradi ya maji jambo linasababisha kupokea miradi isiyokuwa na
viwango mwisho wa siku kuwa miradi hewa kutokana na hali hiyo amewataka kuwa
huru kuhoji na kujua bajeti ya miradi na jinsi inavyotunzwa.
Bwana Andochius Kamuhabwa ni
mwezeshaji kutoka katika shirika hilo amesema kuwa jambo linalofanyika kwa sasa
ni kuona kwanini miradi mingi ya maji inaanzishwa au kuwekezwa kwa Gharama
kubwa lakini baada ya siku haifanyi kazi.
Kamuhabwa amesema kuwa matarajio yao
ni kufika vijijini na kuangalia baadhi ya miradi iliyopo kama inafanya kazi
vizuri na kwa ufanisi na kama haifanyi kazi vizuri lazima zitazamwe changamoto
zinaifanya baadhi ya miradi hiyo kutokamilika.
Hata hivyo wananchi hao wamehimiza kuvitunza vyanzo vya maji kwa kuwa wafuatiliaji katika miradi hiyo.
Shiraka hilo linahudumia kata 6 katika
halmashauri ya wilaya ya Bukoba ambazo ni Ibwera, Katoma, Katoro, Katerero,
Maruku na Kemondo.
No comments:
Post a Comment